-
Nimezeeka na Kushiba SikuMnara wa Mlinzi—2002 | Agosti 1
-
-
Yote hayo yalianza mnamo mwaka wa 1910 nilipopokea zawadi kutoka kwa mama yangu, nikiwa na umri wa miaka kumi.
FAMILIA yetu iliishi katika nyumba ya mbao katika kitongoji cha Crows Nest kilicho Kaskazini ya Sydney. Siku moja nilitoka shuleni nikamkuta mama yangu akizungumza na mwanamume fulani mlangoni. Nilitaka kujua mtu huyo aliyevalia suti na kubeba mkoba uliojaa vitabu ni nani. Kwa sababu ya woga niliomba radhi kisha nikaingia ndani ya nyumba. Hata hivyo, dakika chache baadaye, Mama aliniita. Akasema: “Mtu huyu ana vitabu vizuri, na vyote vinazungumzia Maandiko. Na sasa, kwa sababu karibuni utasherehekea siku yako ya kuzaliwa, ninaweza kukununulia ama nguo mpya au vitabu hivi. Unapenda nini?”
Nami nikamjibu, “O, asante Mama, nitachukua vitabu.”
Kwa hiyo, nikiwa na umri wa miaka kumi, nikawa na mabuku matatu ya kwanza ya Studies in the Scriptures yaliyoandikwa na Charles Taze Russell. Kwa sababu singeweza kuelewa vitabu hivyo kwa urahisi, yule mwanamume alieleza kwamba mama alihitaji kunisaidia kuvielewa. Mama akasema kwamba angefurahi kufanya hivyo.
-
-
Nimezeeka na Kushiba SikuMnara wa Mlinzi—2002 | Agosti 1
-
-
Jirani Aniambia Kweli za Kiroho
Kwa miaka yote hiyo, nilisafiri na “vitabu vya Biblia.” Ijapokuwa sikuwa nimevisoma, moyoni mwangu nilijua kwamba vilikuwa na ujumbe wa maana. Halafu, siku moja mwishoni mwa miaka ya 1920, jirani yetu Lil Bimsom, alitutembelea. Tukaenda mezani, tukaketi na kunywa chai.
Ghafula alishangaa na kusema, “Kumbe una vitabu hivyo!”
Vitabu vipi? nikauliza kwa mshangao.
Akaelekezea kidole vitabu Studies in the Scriptures vilivyokuwa kwenye maktaba. Lil aliviomba akaenda navyo nyumbani na kuvisoma kwa makini. Punde si punde, msisimuko wake kuhusu aliyosoma ukawa wazi.
-