-
Jinsi ya Kukabiliana na KigugumiziAmkeni!—2010 | Mei
-
-
Msaada kwa Walio na Kigugumizi
Jambo la kushangaza ni kwamba watu wenye kigugumizi wanaweza kuimba, kunong’ona, kujizungumzia au kuzungumza na wanyama wao vipenzi, kuzungumza wakati uleule na wengine, au kuwaiga wengine bila tatizo lolote. Isitoshe, asilimia 80 ya watoto wenye kigugumizi huacha kuwa na tatizo hilo bila kutibiwa. Namna gani hiyo asilimia 20 inayosalia?
Leo kuna matibabu ya kuwafunza watu kuzungumza kwa ufasaha zaidi. Mbinu fulani zinahusisha kulegeza taya, midomo, na ulimi na kupumua kutoka kwenye kiwambo. Pia wagonjwa wanaweza kufundishwa kuvuta pumzi kwa kiasi kidogo kutoka kwenye kiwambo na kisha kupumua polepole wanapozungumza. Pia, wanaweza kutiwa moyo kuvuta vokali na konsonanti fulani wanapozungumza. Mgonjwa huanza kuzungumza haraka kadiri ufasaha wake unavyoboreka.
Mtu anaweza kujifunza ustadi huo kwa saa chache tu. Lakini kutumia mbinu hizo kwa mafanikio chini ya hali zenye mkazo sana huenda kukahusisha kufanya mazoezi kwa saa nyingi sana.
-
-
Jinsi ya Kukabiliana na KigugumiziAmkeni!—2010 | Mei
-
-
b Ingawa maoni mbalimbali kuhusu visababishi na matibabu yanayofaa ya kigugumizi yanafanana, hayapatani nyakati zote. Gazeti Amkeni! halipendekezi maoni au matibabu yoyote hususa.
c Katika visa fulani, huenda wataalamu wakapendekeza kifaa fulani cha kuzuia kigugumizi ambacho hufanya sikio lichelewe kusikia.
-