Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuteseka Kwingi Mno
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Februari 15
    • Sehemu ya Ubuni wa Mungu?

      Je, yawezekana, kama vile wengine wamedai, kwamba kuteseka huku kusikokoma ni sehemu ya ubuni wa Mungu usioweza kufahamika? Je, ni lazima tuteseke sasa ili tuthamini uhai ‘katika ulimwengu unaofuata’? Je, ni kweli kama vile mwanafalsafa Mfaransa Teilhard de Chardin alivyoamini, kwamba “kuteseka kunakoua na kuvunjavunja, ni kwa lazima kwa binadamu ili aishi na kuwa roho”? (The Religion of Teilhard de Chardin; italiki ni zetu.) Bila shaka la!

      Je, mbuni mwenye ufikirio angeumba kimakusudi mazingira yenye kufisha kisha adai kuwa mwenye huruma alipowaokoa watu kutoka kwa matokeo yayo? La hasha! Kwa nini Mungu mwenye upendo afanye jambo kama hilo? Kwa hiyo, kwa nini Mungu anaruhusu kuteseka? Je, kuteseka kutapata kwisha? Makala ifuatayo itazungumzia maswali haya.

  • Kuteseka Kutakapokuwa Hakupo Tena
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Februari 15
    • KUTESEKA hakukuwa sehemu ya kusudi la Mungu la awali kwa familia ya kibinadamu. Hakubuni kuteseka wala hakutaki. ‘Ikiwa ni hivyo,’ huenda ukauliza, ‘kulianzaje, na kwa nini Mungu amekuruhusu kuendelee hata sasa?’—Linganisha Yakobo 1:13.

      Jibu lapatikana katika rekodi ya mapema zaidi ya historia ya mwanadamu, Biblia, hasa kitabu cha Mwanzo. Chasema kwamba wazazi wetu wa kwanza, Adamu na Hawa, walimfuata Shetani Ibilisi katika uasi wake dhidi ya Mungu. Matendo yao yalizusha masuala ya msingi yaliyoshambulia msingi wenyewe wa sheria na utaratibu wa ulimwengu wote mzima. Walipodai haki ya kujiamulia lililokuwa jema na lililokuwa baya, walisai enzi kuu ya Mungu. Walisaili haki yake ya kutawala na kuwa mwamuzi pekee wa “mema na mabaya.”—Mwanzo 2:15-17; 3:1-5.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki