Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Hatimaye, katika 1940, Mahakama ilisikiliza kikamili kesi iliyoitwa Minersville School District v. Gobitis.k Kundi kubwa la mawakili mashuhuri walitoa hoja katika kesi hiyo kwa pande zote. J. F. Rutherford alitoa hoja ya maneno kwa niaba ya Walter Gobitas na watoto wake. Mshiriki wa idara ya sheria ya Chuo Kikuu cha Harvard aliwakilisha Shirika la Mawakili wa Marekani na Chama cha Kutetea Uhuru wa Raia katika kutoa hoja dhidi ya kusalimu bendera kwa lazima. Hata hivyo, hoja zao zilikataliwa, na kukiwa na mmoja tu aliyekuwa na maoni tofauti, Mahakama Kuu Zaidi iliamua mnamo Juni 3, kwamba watoto ambao hawangesalimu bendera wangefukuzwa kutoka shule za umma.

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • k 310 U.S. 586 (1940). Walter Gobitas (mwendelezo sahihi), aliyekuwa baba, pamoja na watoto wake William na Lillian, walikuwa wameenda mahakamani ili kuzuia baraza la shule lisiwakataze watoto hao wawili kuhudhuria shule ya umma ya Minersville kwa sababu watoto hao hawangeisalimu bendera ya taifa. Mahakama ya wilaya ya taifa na mahakama ya mzunguko ya rufani pia ziliamua kwa kuwapendelea Mashahidi wa Yehova. Kisha baraza la shule likakata rufani ya kesi hiyo kwa Mahakama Kuu Zaidi.

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku katika ukurasa wa 684]

      Ushahidi kwa Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani

      Alipotokea mbele ya Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani akiwa mshauri wa kisheria katika kesi ya “Gobitis,” Joseph F. Rutherford, mshiriki wa Shirika la Mawakili wa New York na msimamizi wa Watch Tower Society, alikazia fikira waziwazi juu ya umaana wa kujinyenyekeza kwa utawala wa Yehova Mungu. Yeye alisema:

      “Mashahidi wa Yehova ni wale wanaotoa ushuhuda kwa jina la Mungu Mweza Yote, ambaye jina lake pekee ni YEHOVA. . . .

      “Ninaelekeza fikira kwenye uhakika wa kwamba Yehova Mungu, aliahidi miaka zaidi ya elfu sita iliyopita, juu ya kusimamisha serikali ya uadilifu kupitia Mesiya. Atatimiza ahadi hiyo kwa wakati wake. Mambo ya hakika ya siku za leo kulingana na unabii yanaonyesha kwamba wakati huo u karibu. . . .

      “Mungu, Yehova, ndiye chanzo pekee cha uhai. Hakuna mtu mwingine anayeweza kutoa uhai. Jimbo la Pennsylvania haliwezi kutoa uhai. Serikali ya Amerika haiwezi. Mungu alifanya sheria hii [kukataza ibada ya sanamu], kama vile Paulo anavyosema, ili kulinda salama watu Wake na ibada ya sanamu. Mnasema hilo ni jambo dogo. Na ndivyo lilivyokuwa lile tendo la Adamu la kula tunda lililokatazwa. Si lile tofaa alilokula Adamu, bali ni lile tendo lake la kutomtii Mungu. Suala ni ikiwa mwanadamu atamtii Mungu au atatii mfumo fulani wa kibinadamu. . . .

      “Ninakumbusha Mahakama hii (si lazima nifanye hivyo) kwamba katika kesi ya ‘Church v. United States’ Mahakama hii ilisema kwamba Amerika ni taifa la Kikristo; na hiyo inamaanisha kwamba ni lazima Amerika itii sheria ya Kimungu. Pia inamaanisha kwamba Mahakama hii inatambua kisheria uhakika wa kwamba sheria ya Mungu ndiyo kuu zaidi. Na ikiwa mtu anaamini kwa kudhamiria kwamba sheria ya Mungu ni kuu zaidi na anajiendesha mwenyewe kwa kudhamiria kulingana nayo, hakuna mamlaka ya kibinadamu inayoweza kudhibiti au kuingilia dhamiri yake. . . .

      “Naomba nikubaliwe kuelekeza fikira kwenye jambo hili: kwamba mwanzoni mwa kila kikao cha Mahakama hii mtangazaji hutangaza maneno haya: ‘Mungu okoa Marekani na Mahakama hii inayoheshimika.’ Na sasa ninasema, Mungu okoa Mahakama hii inayostahika isitende kosa litakaloongoza watu hawa wa Marekani kuwa jamii yenye mamlaka kamili na kuharibu uhuru wote unaohakikishiwa na Katiba. Hili ni jambo lililo takatifu kwa kila Mwamerika anayempenda Mungu na Neno Lake.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki