Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Hatimaye, katika Mei 3, 1943, katika kesi ya maana sana ya Murdock v. Commonwealth of Pennsylvania,a Mahakama Kuu Zaidi ilibatilisha uamuzi wayo wa kwanza katika kesi ya Jones v. Opelika. Ilijulisha kwamba kodi yoyote ya leseni inayoitishwa kwanza ili mtu aweze kuwa na uhuru wa dini wa kugawanya fasihi za kidini ni jambo lisilo la kikatiba. Kesi hiyo iliandaa fursa kwa Mashahidi wa Yehova katika Marekani na imerejezewa kuwa kiolezo katika mamia ya kesi tangu wakati huo.

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku katika ukurasa wa 688]

      “Aina ya Uenezaji-Evanjeli wa Wamishonari Ulio wa Kikale”

      Katika 1943, katika kesi ya “Murdock v. Pennsylvania,” Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani ilisema hivi, miongoni mwa mambo mengine:

      “Kugawanywa kwa trakti za kidini kwa mkono ni aina ya uenezaji-evanjeli wa wamishonari ulio wa kikale—wa kale kama historia ya matbaa ya uchapaji. Kumekuwa kani yenye nguvu katika mashirika mbalimbali ya kidini kwa muda wa miaka mingi. Aina hiyo ya uenezaji-evanjeli inatumiwa leo kwa kiwango kikubwa na mafarakano mbalimbali ya kidini ambayo makolpota wayo hupeleka Gospeli kwa maelfu na maelfu ya makao na hutafuta kupata wenye kushikamana na imani yao kupitia ziara za kibinafsi. Ni zaidi ya kuhubiri; ni zaidi ya kugawanya fasihi za kidini. Ni jumla ya hayo yote mawili. Kusudi layo ni kueneza evanjeli kama lile la mkutano wa kuhuisha. Aina hiyo ya utendaji wa kidini ni ya cheo kilekile cha juu chini ya Rekebisho la Kwanza kama vile ibada katika makanisa na mahubiri kutoka kwa mimbari. Hudai ulinzi uleule ambao utendaji mwingineo wa kidini unaokubalika na ulio wa kawaida hupewa. Pia hudai uhakikisho wa uhuru wa usemi na uhuru wa uandishi kama ule mwingineo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki