-
Historia ya Maumivu ya MenoAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
Dawa ya kutia ganzi iliyotengenezwa kutokana na oksidi-nitrasi au gesi ya kuwafanya watu wacheke, iligunduliwa muda mfupi baada ya mwanakemia Mwingereza Joseph Priestley kuitayarisha mnamo 1772. Lakini hakuna aliyeitumia kama dawa ya kutia ganzi hadi mwaka wa 1844. Desemba 10 mwaka huo, Horace Wells, daktari kutoka Hartford, Connecticut, Marekani, alihudhuria mkutano ambao wale waliovuta gesi hiyo waliwatumbuiza watu. Wells aliona kwamba mtu aliyeathiriwa na gesi hiyo alikwaruza mguu wake kwenye benchi ngumu bila kuhisi maumivu. Wells alikuwa mwanamume mwenye huruma na hivyo alihisi uchungu kwa maumivu aliyowasababishia wagonjwa wake. Mara moja alifikiria kutumia gesi hiyo kutia ganzi. Lakini kabla ya kuitumia kwa wengine, aliamua kuitumia yeye mwenyewe. Siku iliyofuata, aliketi kwenye kiti chake na kuvuta gesi hiyo hadi akapoteza fahamu. Kisha daktari mwenzake akang’oa gego lake. Hilo lilikuwa tukio muhimu katika historia. Mwishowe, mbinu ya kufanya upasuaji bila maumivu ilikuwa imepatikana!a
-
-
Historia ya Maumivu ya MenoAmkeni!—2007 | Septemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 29]
Picha iliyochorwa na msanii kuonyesha matibabu ya kwanza ya meno kwa kutumia oksidi-nitrasi kutia ganzi, mwaka wa 1844
[Picha zimenandaliwa na]
Courtesy of the National Library of Medicine
-