Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Maadili Yanazorota?
    Amkeni!—2003 | Juni 8
    • Maadili Mengine Yanayozorota

      Maadili mengine ambayo yamekuwapo kwa miaka mingi yanazorota pia. Uchunguzi wa Maadili Ulimwenguni, ulioongozwa na Profesa Inglehart, unaonyesha kwamba katika nchi zilizoendelea watu “wanazidi kudharau mamlaka.”

      Tangu jadi watu wamekuwa na maadili ya kuwajibika kazini. Lakini kuna uthibitisho kwamba maadili hayo pia yanazorota. Huko Marekani, Shirika la Kitaifa la Wafanyabiashara wa Kujitegemea liliwachunguza waajiri zaidi ya nusu milioni. “Asilimia 31 walisema kwamba ni vigumu kujaza nafasi za kazi zilizo wazi, na asilimia 21 walisema kwamba kwa ujumla, kazi haifanywi vizuri.” Mwajiri mmoja alisema hivi: “Inaendelea kuwa vigumu kupata wafanyakazi ambao wanataka kufanya kazi kwa zaidi ya siku moja, wanaofika kazini bila kuchelewa, na ambao hawajalewa.”

      Huenda hali hiyo inaletwa na sababu za kiuchumi. Faida ya biashara inapopungua, wafanyakazi wanafutwa au wanapunguziwa marupurupu fulani. Gazeti Ethics & Behavior linasema hivi: “Wafanyakazi wenye waajiri kama hao wasio waaminifu na wasiowajibika, huanza kuwa na maoni yasiyofaa kuwaelekea. Hawawezi kufanya kazi kwa bidii kwa sababu huenda kesho wakafutwa.”

      Nidhamu na adabu ni mambo mengine ambayo yamezorota sana. Uchunguzi uliofanywa nchini Australia ulifikia mkataa huu: “Zaidi ya asilimia 87.7 ya wafanyakazi walisema [kwamba] utovu wa nidhamu unapunguza bidii kazini.” Wafanyabiashara mashuhuri nchini Marekani walipohojiwa, “asilimia themanini kati yao walisema kuna ongezeko la matusi katika biashara.” Kulingana na shirika la habari la CNN, “wateja wengi hawahudumiwi vizuri na karibu nusu ya wale waliohojiwa walisema kwamba iliwabidi waondoke dukani bila kununua chochote mwaka uliopita. Nusu yao walisema kwamba wao huwaona watu wakizungumza kwa simu ya mkononi kwa sauti kubwa au kwa njia yenye kuudhi. Pia madereva sita kati ya 10 walisema kwamba wao huwaona wengine wakiendesha gari bila kujali.”

      Je, Uhai wa Mwanadamu Una Thamani?

      Wakati mwingine, watu husema kwamba wanafuata “maadili” fulani, lakini hawatendi kulingana na maneno yao. Kwa mfano, Taasisi ya Maadili Duniani ilifanya kura ya maoni katika nchi 40. Asilimia 40 walisema “kuheshimu uhai” ni mojawapo ya maadili matano “yaliyo muhimu zaidi.”a

  • Je, Maadili Yanazorota?
    Amkeni!—2003 | Juni 8
    • Watu walipoulizwa, “Ni kitu gani chenye umuhimu mdogo zaidi maishani?” katika kura ya maoni ya Gallup, wengi walisema moja kati ya mambo mawili yenye umuhimu mdogo sana ni ‘kuwa mwaminifu kwa dini yao.’ Basi si ajabu kwamba watu wanaoenda kanisani wanazidi kupungua. Profesa Inglehart anasema kwamba nchi za Magharibi “zinawafanya watu wahisi wakiwa salama sana” na kwamba jambo hilo “limepunguza uhitaji wa usalama waliopata katika dini zamani.”

      Kadiri watu wanavyoacha dini, ndivyo wanavyoendelea kukosa imani katika Biblia. Katika uchunguzi mmoja wa kimataifa, watu waliulizwa walipata mwongozo kutoka kwa nani au kutoka wapi walipotaka kujua mambo yanayofaa au yasiyofaa. Wengi sana walisema walitegemea ujuzi wao maishani. “Ni wachache sana waliosema kwamba walitegemea neno la Mungu,” yasema ripoti ya uchunguzi huo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki