-
Jina la Mungu Lajulishwa Katika KiswahiliMnara wa Mlinzi—2012 | Septemba 1
-
-
Inaaminika ya kwamba Kiswahili kimekuwa kikizungumzwa tangu karne ya kumi. Lugha hiyo ilianza kuandikwa katika karne ya 16. Watu wanaojifunza Kiswahili wanatambua kwamba baadhi ya maneno yana asili ya Kiarabu. Asilimia 20 ya maneno ya Kiswahili yana asili ya Kiarabu, na asilimia inayobaki yana asili ya Kiafrika. Hivyo, haishangazi kwamba kwa mamia ya miaka Kiswahili kilikuwa kikiandikwa kwa herufi za Kiarabu.
-
-
Jina la Mungu Lajulishwa Katika KiswahiliMnara wa Mlinzi—2012 | Septemba 1
-
-
Krapf alikuwa wa kwanza kutumia herufi za Kiroma katika kuandika Kiswahili badala ya herufi za Kiarabu zilizotumiwa na watu wengi. Kati ya sababu alizotoa za kutotumia herufi za Kiarabu ni kwamba “herufi za Kiarabu zingewatatanisha watu kutoka Ulaya” ambao baadaye wangejifunza lugha hiyo na pia “herufi za Kiroma zingewasaidia ‘Wenyeji katika kujifunza lugha za Ulaya.’” Herufi za Kiarabu ziliendelea kutumiwa kwa miaka mingi; sehemu fulani za Biblia zilichapishwa katika herufi hizo.
-