-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
James na Dawne Hockett, ni wamishonari katika jiji kuu la Swaziland, Mbabane. James alihitimu Shule ya Gileadi mwaka wa 1971, naye Dawne alihitimu mwaka wa 1970. James alitumia mfano huu kuonyesha jinsi wamishonari wanavyolazimika kujifunza desturi mbalimbali: “Tulikuwa tukihubiri katika eneo ambalo halijagawiwa yeyote, naye chifu akawakusanya watu na kuniomba niwahutubie. Tulikuwa mahali ambapo ujenzi ulikuwa ukiendelea, na mawe ya kujengea yalikuwa yametapakaa. Kulikuwa na unyevunyevu, hivyo nikakalia jiwe moja, naye Dawne akaketi karibu na mimi kwenye jiwe hilo. Dada mmoja Mswazi alimwita Dawne na kumwomba aketi karibu naye. Dawne akamwambia kwamba yuko sawa, lakini dada huyo akasisitiza. Baadaye, tulielezwa kwamba kwa kuwa baadhi ya wanaume walikuwa wameketi chini kabisa, wanawake hawakupaswa kuketi juu kuliko wanaume. Hiyo ndiyo desturi huko mashambani.”
James na Dawne walitembelea shule fulani kuzungumza na mwalimu mmoja anayependezwa. Mwalimu huyo alimtuma mwanafunzi awaambie kwamba hangeweza kuzungumza nao wakati huo. Basi, wakaamua kuzungumza na mvulana huyo, anayeitwa Patrick. Walimuuliza ikiwa anajua ni kwa nini wamekuja. Baada ya mazungumzo, walimpa kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi na kuanza kujifunza Biblia pamoja naye. Patrick alikuwa yatima aliyekuwa akiishi katika chumba kilichokuwa karibu na nyumba ya baba yake mdogo. Alilazimika kujitunza, kujipikia, na kufanya kazi ya muda ili ajilipie karo ya shule. Alifanya maendeleo, akabatizwa, na sasa ni mzee kutanikoni.
-
-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
James na Dawne Hockett
-