Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na mwingine akatokea, farasi wa rangi-moto; na yule mmoja aliyeketi juu yake alipewa ruhusa ya kuondolea mbali amani kutoka dunia ili wao wapaswe kuchinja mmoja na mwenzake; na upanga mkubwa akapewa yeye.” (Ufunuo 6:4, NW)

  • Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 16. Ni lini na jinsi gani mpandaji-farasi mwekundu alipewa “upanga mkubwa”?

      16 Kulikuwa kumekuwa na vita vingi kabla ya 1914, ule mwaka Mpandaji-farasi mweupe alipopokea taji lake. Lakini sasa mpandaji-farasi mwekundu anapewa “upanga mkubwa.” Hiyo inadokeza nini? Kwa mlipuko wa Vita ya Ulimwengu 1, vita vya binadamu vimekuwa vyenye umwagaji-damu mwingi zaidi, vyenye uharibifu mwingi zaidi ya vilivyopata kuwa kabla ya hapo. Wakati wa mwosho-damu wa 1914-18, matanki, gesi zenye sumu, eropleni, sabmarini, mizinga mikubwa, na silaha za otomatiki zilitumiwa ama kwa mara ya kwanza ama kwa kadiri isiyotangulia kufanywa. Katika mataifa yapata 28, idadi ya watu wa nchi kwa ujumla, si wale tu ambao kazi yao ya maisha ni askari-jeshi, walisukumizwa kwenye jitihada za vita. Majeruhi walikuwa kadiri ya kuogopesha. Askari-jeshi zaidi ya milioni tisa walichinjwa, na majeruhi ya raia walikuwa wengi mno. Hata ilipokwisha vita, hakukuwa na kurudia amani halisi duniani. Zaidi ya miaka 50 baada ya vita, Konrad Adenauer waziri wa serikali Mjeremani alitoa elezo hili: “Usalama na utulivu vimetoweka katika maisha ya watu tangu 1914.” Kweli kweli yule mpandaji-farasi wa rangi-moto alipewa ruhusa aondolee mbali amani duniani!

      17. Utumizi wa huo “upanga mkubwa” umeendeleaje, kufuata Vita ya Ulimwengu 1?

      17 Halafu, kiu yake ya kutaka kuona damu ikimwagwa ikiwa imechochewa, yule mpandaji-farasi mwekundu alijitumbukiza ndani ya Vita ya Ulimwengu 2. Zana za uchinjaji zilizidi kuwa za kishetani zaidi, nayo majeruhi yakapanda juu kuwa mara nne ya yale ya Vita ya Ulimwengu 1. Katika 1945 bomu mbili za atomu zililipuka juu ya Japani, kila mojapo ilifutilia mbali—kwa dharuba moja—makumi ya maelfu ya majeruhi. Katika pindi ya vita ya pili ya ulimwengu, yule mpandaji-farasi mwekundu alivuna mavuno makubwa ya maisha zapata milioni 55, na hata wakati huo yeye hakutosheka. Imeripotiwa kwa njia yenye kuaminika kwamba nafsi zaidi ya milioni 20 zimeanguka chini ya ule “upanga mkubwa” tangu Vita ya Ulimwengu 2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki