Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?
    Amkeni!—2005 | Septemba 8
    • Ushirikiano Husaidia Katika Uzalishaji

      Nyuki anapotua juu ya ua, yeye huanza kushirikiana na ua hilo. Nyuki huyo hupata nekta na chavua na wakati huohuo ua hupata chavua kutoka kwenye maua mengine ya aina hiyo. Upatano huo huwezesha ua kuzaa. Baada ya kuchavushwa, maua huacha kutengeneza chakula. Wadudu hujuaje kwamba wakati wa kula umekwisha? Maua “huwajulisha” kwa njia mbalimbali. Huenda yakapoteza harufu, yakaangusha petali, au yakakua kuelekea upande tofauti au kubadili rangi, labda kuwa na rangi hafifu. Huenda jambo hilo likatusikitisha, lakini kufanya hivyo huwasaidia sana nyuki wanaofanya kazi kwa bidii kwani sasa wanaweza kuelekeza jitihada zao kwenye mimea ambayo bado haijanyauka.

      Katika miaka ya hivi karibuni, idadi ya wachavushaji, hasa nyuki, imepungua sana katika maeneo fulani. Hali hiyo inatia wasiwasi kwani karibu asilimia 70 ya maua hutegemea wadudu kwa ajili ya uchavushaji. Isitoshe, asilimia 30 ya vyakula tunavyotumia hutokana na mazao yaliyochavushwa na nyuki.

  • Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?
    Amkeni!—2005 | Septemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 7]

      Nyuki huwezesha maua yazae

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki