-
Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?Amkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
“Hakuna kiumbe anayejitegemea. Kila kiumbe ana uhusiano na viumbe wengine kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja.”—“Symbiosis—An Introduction to Biological Associations.”
“MFUMO wa viumbe.” Huo ni ufafanuzi unaofaa kwelikweli, kwani uhai umefanyizwa kwa mtandao wa viumbe wanaoshirikiana na kutegemeana! Wanadamu ni sehemu ya mfumo huo. Ili kuthibitisha hilo, unahitaji tu kutazama mwili wako. Bakteria nyingi zisizoweza kuonekana hufanya kazi ndani ya mfumo wako wa umeng’enyaji na kukusaidia uwe na afya nzuri kwa kuharibu viumbe wanaoweza kukudhuru na kukusaidia kumeng’enya chakula na kutokeza vitamini muhimu. Kwa upande mwingine, wewe huandalia bakteria hizo chakula na mazingira yanayofaa.
Kuna ushirikiano kama huo kati ya wanyama, hasa wale wanaocheua kama vile ng’ombe, mbawala, na kondoo. Sehemu ya kwanza ya tumbo lao lililogawanywa katika sehemu nyingi, ina mfumo halisi wa ikolojia wa bakteria, kuvu, na protozoa. Kupitia uchachushaji, viumbe hao wadogo huvunja-vunja selulosi, ambayo ni wanga wenye nyuzinyuzi ulio katika mimea, na kutokeza virutubisho mbalimbali. Hata wadudu fulani ambao hula selulosi, kama vile jamii za mbawakawa, mende, samaki-sanduku, mchwa, na nyigu, hutumia bakteria ili kumeng’enya chakula.
Inapendeza kuona ushirikiano wa karibu kama huo kati ya viumbe wasiofanana lakini wanaoishi pamoja.a “Mapatano kama hayo ni muhimu kwa ukuzi wa kila kiumbe,” anasema Tom Wakeford katika kitabu chake Liaisons of Life.
-
-
Kwa Nini Ushirikiano Ni Muhimu?Amkeni!—2005 | Septemba 8
-
-
a Viumbe hushirikiana katika njia tatu: njia ya kwanza viumbe wote wawili hunufaika; njia ya pili kiumbe mmoja hunufaika bila kumdhuru kiumbe yule mwingine; na njia ya tatu kiumbe mmoja hunufaika na kumdhuru yule mwingine. Makala hii itazungumzia mifano kuhusu ushirikiano ambao viumbe wote wawili hunufaika.
-