Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Historia Inayopendeza ya Siria
    Amkeni!—2003 | Februari 8
    • Jiji la Jangwani la Palmyra

      Inachukua saa tatu kufikia jiji la kale la Palmyra kwa gari, lililoko kaskazini-mashariki ya Damasko. Jiji hilo linaitwa Tadmori katika Biblia. (2 Mambo ya Nyakati 8:4) Jiji hilo lilikuwa katikati ya Bahari ya Mediterania na Mto Eufrati na linapata maji kutoka chemchemi za chini ya ardhi zinazobubujika hapo, ambazo zinatoka kwenye milima iliyo upande wa kaskazini. Wanabiashara wa kale waliosafiri kati ya Mesopotamia na nchi za magharibi walipitia eneo la Fertile Crescent upande wa kaskazini, mbali sana na Palmyra. Hata hivyo, katika karne ya kwanza K.W.K., kulikuwa na mgogoro wa kisiasa huko kaskazini hivyo wanabiashara wakaanza kutumia njia nyingine fupi upande wa kusini. Wakati huo Palmyra likaanza kusitawi.

      Kwa kuwa jiji la Palmyra lilitumiwa na Waroma kukinga eneo la mashariki la milki hiyo, likaunganishwa na Siria iliyotawaliwa na Roma, lakini hatimaye lilipata uhuru. Kandokando ya barabara kuu ya fahari yenye nguzo kulikuwa na mahekalu makubwa, tao, vyumba vya kuogea, na jumba la michezo. Njia za miguu pande zote za barabara hiyo zilifunikwa kwa mawe, lakini sehemu ya katikati iliachwa ili ngamia watembee kwa starehe. Misafara ya ngamia iliyosafiri kati ya India na China upande wa Mashariki na Ugiriki na Roma upande wa Magharibi ilitua Palmyra. Hapo walitozwa kodi za vitambaa vya hariri, vikolezo, na bidhaa nyingine walizosafirisha.

      Jiji la Palmyra lilisitawi sana katika karne ya tatu W.K., nalo lilikuwa na wakazi 200,000 hivi wakati huo. Ndipo Malkia Zenobia mwenye kutaka makuu alipopigana na Roma na hatimaye akashindwa mwaka 272 W.K. Hivyo, bila kujua Zenobia alitimiza sehemu ya unabii ulioandikwa na nabii Danieli miaka 800 mapema.a (Danieli, sura ya 11) Baada ya Zenobia kushindwa, Palmyra liliendelea kuwa jiji muhimu katika Milki ya Roma kwa muda, lakini halikuwa na fahari na nguvu kama awali.

  • Historia Inayopendeza ya Siria
    Amkeni!—2003 | Februari 8
    • [Picha katika ukurasa wa 26]

      Palmyra

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki