-
Ugarit—Jiji la Kale Lililokuwa Kwenye Kitovu cha Ibada ya BaaliMnara wa Mlinzi—2003 | Julai 15
-
-
Kwa upande mwingine, Baali ni mungu mwenye nguvu na mwenye kutaka makuu ambaye hutafuta kutawala miungu na wanadamu.
-
-
Ugarit—Jiji la Kale Lililokuwa Kwenye Kitovu cha Ibada ya BaaliMnara wa Mlinzi—2003 | Julai 15
-
-
Katika shairi moja kuhusu ugomvi juu ya uongozi, Baali anamshinda mungu wa bahari, Yamm, ambaye ni mwana mpendwa wa mungu Eli. Ushindi huo labda uliwapa mabaharia wa Ugarit uhakika wa kwamba Baali angeweza kuwalinda baharini. Katika mapambano na Moti, Baali anashindwa na kushuka katika ulimwengu wa chini. Hivyo, ukame unatokea na utendaji mbalimbali wa wanadamu unakoma. Mke wa Baali na dada wa Anati—mungu wa kike wa upendo na vita—anamwua Moti na kumrudishia Baali uhai. Baali anawaangamiza wana wa mke wa mungu Eli, Athariti (Ashera), na anachukua tena utawala. Lakini Moti anarudi baada ya miaka saba.
Watu fulani hueleza shairi hilo kuwa mfano wa mzunguko wa majira mwakani wakati mvua za kutoa uhai zinaposhindwa na joto kali la majira ya joto na kurudi kwa majira ya majani kupukutika. Wengine hufikiri kwamba miaka saba ya mzunguko wa majira inahusiana na woga wa njaa na ukame. Katika hali yoyote ile, ukuu wa Baali ulionekana kuwa muhimu kwa mafanikio ya jitihada za mwanadamu. Mtaalamu Peter Craigie anasema hivi: “Kusudi la dini ya Baali lilikuwa kuhifadhi mamlaka yake; hivyo waabudu wake waliamini kwamba, maadamu tu alibaki mwenye uwezo, mavuno na mifugo ambayo ni muhimu kwa mwanadamu vingeendelea kuhifadhiwa.”
-