Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nuru ya Kiroho Yang’aa Mashariki ya Kati
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 1
    • Shahidi Yousef Rahhal wa Lebanon, aliyekuwa ameishi Marekani kwa miaka mingi alirudi kutembea Lebanon mwaka wa 1936. Alileta vikuza-sauti na santuri mbili. Tukaweka vifaa hivyo juu ya gari aina ya Ford ya mwaka wa 1931, na kusafiri kotekote Lebanon na Syria tukihubiri ujumbe wa Ufalme katika maeneo ya mbali. Kikuza-sauti kilisikika kwa umbali wa kilometa kumi. Watu walipanda hadi kwenye paa za nyumba zao ili wasikie kile walichoamini kuwa sauti kutoka mbinguni. Wale waliokuwa mashambani waliacha kazi zao na kukaribia ili wasikilize.

      Mojawapo ya safari zangu za mwisho pamoja na Yousef Rahhal ilikuwa safari ya kwenda Aleppo, Syria, katika majira ya baridi kali mwaka wa 1937.

  • Nuru ya Kiroho Yang’aa Mashariki ya Kati
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Septemba 1
    • Petros Lagakos na mke wake waliwasili Tripoli mwaka wa 1937. Katika miaka michache iliyofuata, sisi watatu tulihubiri ujumbe wa Ufalme karibu sehemu zote za Lebanon na Syria kwa kuwatembelea watu nyumbani mwao. Wakati Ndugu Lagakos alipokufa mwaka wa 1943, Mashahidi walikuwa wameangaza nuru ya kiroho katika miji na vijiji vingi vya Lebanon, Syria, na Palestina. Nyakati nyingine, karibu watu 30 kati yetu tulianza safari kwa basi au gari saa tisa usiku ili tuhubiri katika maeneo ya mbali.

      Katika miaka ya 1940, Ibrahim Atiyeh alitafsiri gazeti la Mnara wa Mlinzi katika Kiarabu. Baadaye, mimi nilikuwa nikiandika kwa mkono nakala nne za gazeti hilo na kuzituma kwa Mashahidi kule Palestina, Syria, na Misri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki