Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Kufanyizwa kwa Talmud Mbili

      Hatimaye, kitovu kikuu cha kirabi huko Palestina, kilihamishwa hadi Tiberiasi. Vyuo vingine vya maana vilianzishwa katika Sepphoris, Kaisaria, na Lida. Lakini hali ya kiuchumi iliyokuwa ikidhoofika, misuko-suko ya daima ya kisiasa, na hatimaye mkazo na mnyanyaso kutoka kwa Ukristo wenye kuasi imani ulitokeza kuhama kwa kiwango kikubwa hadi kwenye kitovu kingine chenye idadi kubwa ya Wayahudi, kilichokuwa Mashariki—Babilonia.

      Kwa karne nyingi, wanafunzi walikuwa wametoka kwa wingi huko Babilonia kwenda Palestina ili kujifunza chini ya marabi wakubwa kwenye vyuo. Mmoja wa wanafunzi hao alikuwa Abba ben Ibo, ambaye pia aliitwa Abba Arika—Abba yule mrefu—lakini baadaye alijulikana tu kuwa Rab. Alirudi Babilonia wapata mwaka wa 219 W.K., baada ya kujifunza chini ya Judah ha-Nasi, na kurudi huko kulitia alama wakati wa badiliko la maana kuhusu umuhimu wa kiroho wa jumuiya ya Wayahudi wa Babilonia. Rab alianzisha chuo fulani katika Sura, eneo lililokuwa na Wayahudi wengi lakini wasomi wachache. Sifa yake iliwavuta wanafunzi wa kawaida 1,200 kwenye chuo chake, kukiwa na maelfu zaidi waliohudhuria wakati wa miezi ya Wayahudi ya Adari na Eluli. Samuel, mtu mashuhuri aliyeishi wakati mmoja na Rab, alianzisha chuo katika Nehardea. Vyuo vingine vya muhimu vilianzishwa katika Pumbeditha na Mehoza.

      Sasa hakukuwa na uhitaji wa kusafiri hadi Palestina, kwa kuwa mtu angeweza kujifunza chini ya wasomi wakuu katika Babilonia. Kufanyizwa kwa Mishnah ikiwa maandishi yaliyochanganywa na mengine kulitayarisha njia ya kuwa na vyuo vya Babilonia vilivyojitegemea kabisa. Ijapokuwa mitindo na njia tofauti za kujifunza sasa zilisitawi katika Palestina na Babilonia, kuwasiliana mara nyingi na kubadilishana walimu kulihifadhi muungano wa vyuo hivyo.

  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Huku vyuo vilivyokuwa Palestina vikipungua, Wafasiri wa Babilonia walikuwa wakifikia upeo wa uwezo wao mbalimbali. Abaye na Raba waliendeleza mjadala tata na wenye hila uliopata kuwa bishano ambalo baadaye, lilipata kuwa kigezo cha mchanganuo wa Talmud. Kisha, Ashi, mkuu wa chuo katika Sura (371-427 W.K.), akaanza kukusanya na kuhariri mihtasari ya mijadala. Kulingana na Steinsaltz, alifanya hivyo “akiogopa kwamba, habari nyingi sana za mdomo zilizokosa mpango, zilikuwa hatarini mwa kutoweka kabisa.”

      Habari hiyo nyingi mno haingeweza kupangwa na mwanamume mmoja au hata kizazi kimoja. Kipindi cha Wafasiri katika Babilonia kiliisha katika karne ya tano W.K., lakini kazi ya mwisho ya kuhariri Talmud ya Babilonia iliendelezwa hadi karne ya sita W.K. na kikundi kilichoitwa Saboraim, neno la Kiaramu linalomaanisha “waelezaji,” au “wenye maoni.” Wahariri hao wa mwisho waliunda na kuandika mamia ya mihtasari mbalimbali na kuifanya Talmud ya Babilonia iliyo kamili, wakiipa mtindo na muundo wa maandishi ulioifanya kuwa tofauti na maandishi mengine yote ya Kiyahudi.

  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Zile Talmud Mbili—Je, Zalinganaje?

      Neno la Kiebrania “Talmud” humaanisha “kuchunguza” au “kujifunza.” Wafasiri wa Palestina na wa Babilonia walikuwa wamekusudia kuichunguza, au kuichanganua, Mishnah. Talmud zote mbili (ya Palestina na ya Babilonia) hufanya hivyo, lakini zalinganaje? Jacob Neusner aandika hivi: “Talmud ya kwanza huchanganua uthibitisho, ya pili huchunguza kauli; ya kwanza hubaki katika mambo yaliyochunguzwa, ile ya pili haifanyi hivyo kabisa.”

      Uhariri wenye umakini na mkamilifu zaidi wa Talmud ya Babilonia, uliifanya iwe kubwa zaidi na pia, yenye kina na yenye kupenya zaidi katika mtindo wake wa wazo na mchanganuo. Neno “Talmud” litajwapo, kwa kawaida humaanisha Talmud ya Babilonia. Hiyo ndiyo Talmud ambayo imechunguzwa na kuelezwa zaidi katika karne zote. Kwa maoni ya Neusner, Talmud ya Palestina “iliandikwa na mtu mwenye uhodari,” nayo Talmud ya Babilonia “iliandikwa na mtu mwenye kipaji.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki