Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Hatimaye, kitovu kikuu cha kirabi huko Palestina, kilihamishwa hadi Tiberiasi. Vyuo vingine vya maana vilianzishwa katika Sepphoris, Kaisaria, na Lida. Lakini hali ya kiuchumi iliyokuwa ikidhoofika, misuko-suko ya daima ya kisiasa, na hatimaye mkazo na mnyanyaso kutoka kwa Ukristo wenye kuasi imani ulitokeza kuhama kwa kiwango kikubwa hadi kwenye kitovu kingine chenye idadi kubwa ya Wayahudi, kilichokuwa Mashariki—Babilonia.

  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Mwishoni mwa karne ya nne na mwanzoni mwa karne ya tano W.K., hali ilipata kuwa ngumu hasa kwa Wayahudi waliokuwa katika Palestina. Vizuizi vingi mno na mnyanyaso chini ya mamlaka iliyokuwa ikiibuka ya Jumuiya ya Wakristo yenye kuasi imani lilitokeza kuchukuliwa kwa hatua ya mwisho ya kubatilisha Sanhedrini na wadhifa wa Nasi (mwanzilishi), wapata mwaka wa 425 W.K. Kwa hiyo Wafasiri wa Palestina walianza kuunganisha pamoja mihtasari ya mijadala ya vyuo kuwa kazi yenye upatano ili wahakikishe kuhifadhiwa kwake. Kazi hiyo iliyotungwa kwa haraka mwishoni mwa karne ya nne W.K., ilipata kujulikana kuwa Talmud ya Palestina.b

  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • b Talmud ya Palestina yajulikana sana kuwa Talmud ya Yerusalemu. Hata hivyo, neno hilo limetumiwa kimakosa, kwa kuwa Wayahudi hawakuruhusiwa kuingia Yerusalemu wakati wa kipindi cha Wafasiri.

  • Talmud Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Mei 15
    • Zile Talmud Mbili—Je, Zalinganaje?

      Neno la Kiebrania “Talmud” humaanisha “kuchunguza” au “kujifunza.” Wafasiri wa Palestina na wa Babilonia walikuwa wamekusudia kuichunguza, au kuichanganua, Mishnah. Talmud zote mbili (ya Palestina na ya Babilonia) hufanya hivyo, lakini zalinganaje? Jacob Neusner aandika hivi: “Talmud ya kwanza huchanganua uthibitisho, ya pili huchunguza kauli; ya kwanza hubaki katika mambo yaliyochunguzwa, ile ya pili haifanyi hivyo kabisa.”

      Uhariri wenye umakini na mkamilifu zaidi wa Talmud ya Babilonia, uliifanya iwe kubwa zaidi na pia, yenye kina na yenye kupenya zaidi katika mtindo wake wa wazo na mchanganuo. Neno “Talmud” litajwapo, kwa kawaida humaanisha Talmud ya Babilonia. Hiyo ndiyo Talmud ambayo imechunguzwa na kuelezwa zaidi katika karne zote. Kwa maoni ya Neusner, Talmud ya Palestina “iliandikwa na mtu mwenye uhodari,” nayo Talmud ya Babilonia “iliandikwa na mtu mwenye kipaji.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki