Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Fundisha kwa Ufahamu Wenye Kina na Ushawishi
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • 4. Kwa nini ni lazima wazee Wakristo wawe wasikilizaji wazuri?

      4 Ni muhimu hasa kwa wazee Wakristo kuwa wasikilizaji wazuri. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo kwa kweli wanaweza “kujua jinsi [wapaswavyo] kumpa jibu kila mmoja.” (Wakolosai 4:6) Mithali 18:13 yaonya hivi: “Yeye ajibuye kabla hajasikia, ni upumbavu na aibu kwake.” Wakati mmoja ndugu wawili waliokuwa na nia nzuri walimpa dada shauri kuhusu mambo ya kilimwengu kwa kuwa alikosa mikutano kadhaa. Dada huyo aliumizwa sana kwa sababu hawakumwuliza kwa nini hakuwepo. Alikuwa akipata nafuu kutokana na upasuaji uliofanywa karibuni. Basi, ni muhimu jinsi gani kwamba tusikilize kabla ya kutoa shauri!

      5. Wazee wanaweza kushughulikiaje mabishano ambayo huzuka miongoni mwa akina ndugu?

      5 Kwa wazee, kufundisha mara nyingi huhusisha kuwashauri wengine. Hapa, pia, ni muhimu kuwa msikilizaji mzuri. Kusikiliza ni kwa lazima mabishano yanapozuka miongoni mwa Wakristo wenzi. Ni baada tu ya kusikiliza ndipo wazee wawezapo kumwiga “Baba ambaye huhukumu bila ubaguzi wowote.” (1 Petro 1:17) Mara nyingi hisia-moyo huwa kali sana katika hali kama hizo, na mzee apaswa kukumbuka shauri la Mithali 18:17: “Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa na haki; lakini juani yake huja na kumchunguza.” Mwalimu mwenye matokeo atasikiliza pande zote mbili. Kwa kutoa sala, yeye husaidia kuleta hali ya utulivu. (Yakobo 3:18) Ikiwa hisia-moyo zawa kali sana, huenda akadokeza kwamba kila ndugu amweleze mahangaiko yake moja kwa moja, badala ya hao wawili kuzozana. Kwa kutumia maswali yanayofaa, huenda mzee akabainisha masuala yanayochunguzwa. Katika visa vingi, mawasiliano mabaya, wala si nia ya kudhuru, ndiyo hubainika kuwa kisababishi cha mabishano. Lakini ikiwa kanuni za Biblia zimevunjwa, mwalimu mwenye upendo aweza sasa kufundisha akitumia ufahamu wenye kina, baada ya kusikiliza pande zote mbili.

  • Fundisha kwa Ufahamu Wenye Kina na Ushawishi
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 15
    • 10. Huenda wazee wakatumiaje maswali wanapowasaidia watu mmoja-mmoja ambao wamejeruhiwa kihisia-moyo?

      10 Wazee pia wanaweza kutumia maswali kwa njia nzuri wanapolichunga kundi. Wengi katika kutaniko wamechubuliwa kihisia-moyo na kuumizwa na ulimwengu wa Shetani na huenda wakahisi kwamba wao ni wachafu na wasioweza kupendwa. Huenda mzee akasababu na mtu kama huyo kwa kusema hivi: ‘Ingawa unasema kwamba unahisi wewe ni mchafu, Yehova anahisije kukuhusu? Ikiwa Baba yetu wa kimbingu mwenye upendo alimruhusu Mwana wake afe na kuandaa fidia kwa ajili yako, je, hilo halimaanishi kwamba Mungu anakupenda?’—Yohana 3:16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki