-
Jinsi Unavyoweza Kutunza Meno YakoAmkeni!—2005 | Novemba 8
-
-
Kuoza kwa meno husababishwa na aina mbili za bakteria, yaani, “streptococci na lactobocilli” ambazo hutokeza ukoga, ambao ni utando mwembamba wa bakteria na mabaki ya chakula ambayo hukwama kwenye meno. Bakteria hizo hula sukari na kuigeuza kuwa asidi zinazodhuru ambazo hufanya meno yaoze. Aina fulani za sukari hugeuzwa haraka kuwa asidi au hukwama kwenye meno kwa urahisi, na hivyo kuzipa bakteria hizo muda wa kufanya meno yaoze.b Ukoga ambao hauondolewi unaweza kuwa mgumu kuzunguka fizi.
Kudhibiti ukoga na hasa bakteria za streptococci ni muhimu ili kuzuia meno yasioze. Kwa hiyo, ikiwa ungependa kutunza meno yako, ni lazima usafishe kinywa chako kila siku. Chuo Kikuu cha Upasuaji wa Meno na Kinywa huko Columbia kinasema hivi: “Kuondoa uchafu katikati ya meno kwa kutumia uzi mwembamba pamoja na [kupiga mswaki] ndiyo njia muhimu zaidi ya kudumisha afya ya meno yako na sehemu nyingine zinazoyashikilia.” Picha kwenye ukurasa huu na unaofuata inaonyesha njia moja inayofaa ya kupiga mswaki na kuondoa uchafu katikati ya meno. Daktari wa meno anaweza kupendekeza vifaa na mbinu nyingine ambazo zitakusaidia kusafisha na hivyo kutunza meno yako ifaavyo.
-
-
Jinsi Unavyoweza Kutunza Meno YakoAmkeni!—2005 | Novemba 8
-
-
Madaktari wa meno wanazidi kuzoezwa mbinu za kuzuia kuharibika kwa meno madini yanapoondolewa. Mara nyingi kuoza kwa meno kunaweza kuzuiwa kwa kuziba matundu yanapokuwa bado madogo sana. Kwa hiyo, unapoenda kwa daktari wa meno mapema, unaweza kufurahia matibabu ya meno.
Hata hivyo, asidi inayotokezwa na ukoga ikibaki kwenye meno, meno huanza kuoza. Meno hayo yasipotibiwa, huenda yakawa na matundu. Jino lililo na tundu litahitaji kutibiwa. Ikiwa halijaoza hadi sehemu zenye neva, basi kwa kawaida sehemu iliyooza huondolewa na tundu kuzibwa.
Daktari hutumia kekee kuondoa sehemu iliyooza na kusafisha tundu hilo kisha huliziba. Mchanganyiko wa madini ya zebaki, fedha, na bati unaotumiwa kuziba matundu ya meno huwa mgumu haraka na hushindiliwa ili uenee kwenye tundu lote. Michanganyiko mingine hufanywa iwe migumu kwa kutumia mashini ndogo inayotoa nuru ya buluu. Matundu yasipotibiwa na sehemu zenye neva zianze kuoza, huenda mizizi ikahitaji kuondolewa au hata jino kung’olewa.
-