Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Teknolojia—Fikiria Wengine na Gharama
    Amkeni!—2009 | Novemba
    • ◼ “Kwa hiyo, mambo yote mnayotaka watu wawatendee ninyi, lazima mwatendee wao pia vivyo hivyo.” (Mathayo 7:12) Tukifuata maneno hayo ya Yesu Kristo tunapotumia simu za mkononi na kompyuta, tutawatendea wengine kwa heshima na kuwa na adabu. Mwanamke mmoja anayeitwa Anne anasema hivi: “Mimi na mume wangu tulikuwa katika mkahawa mmoja. Wanaume wawili walikuwa wakila chakula meza iliyokuwa kando yetu. Hata hivyo, mmoja wao alitumia muda wote akizungumza kwenye simu na kula. Tulimhurumia sana mwenzake, ambaye ni kana kwamba alikuwa akila peke yake.” Ungehisije ikiwa ungekuwa pamoja na mwanamume huyo? Ungeumia? Au ungeudhika? Hata kama tunaweza kutumia simu zetu za mkononi mahali popote, wakati wowote, haimaanishi kwamba tufanye hivyo. Kanuni iliyo katika maneno ya Yesu inapaswa kutuongoza.

  • Teknolojia—Fikiria Wengine na Gharama
    Amkeni!—2009 | Novemba
    • [Sanduku katika ukurasa wa 9]

      KUTUMIA SIMU NA KOMPYUTA KWA ADABU

      Unaweza kutumiaje simu ya mkononi na kompyuta kwa njia inayoonyesha kwamba unawajali wengine? Fikiria mambo yafuatayo.

      ◼ Epuka kupiga au kupokea simu wakati na mahali ambapo utawasumbua wengine. Ikiwezekana, zima simu yako.

      ◼ Ikiwa unazungumza na mtu ana kwa ana, usiruhusu simu ikatize mazungumzo hayo isipokuwa iwe lazima kufanya hivyo.

      ◼ Unapozungumza kwenye simu, mkazie fikira yule unayezungumza naye.

      ◼ Usimpige mtu picha kwa kutumia simu yako ya mkononi ikiwa utamkosea heshima au utamwaibisha kwa kufanya hivyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki