-
Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali NgumuAmkeni!—2007 | Machi
-
-
Mabadiliko Makubwa ya Kijamii
Katika miaka ya karibuni, teknolojia imetokeza mabadiliko makubwa ambayo yamewaathiri sana vijana. Kwa mfano, katika nchi nyingi vijana huona simu za mkononi na kompyuta kuwa vyombo muhimu sana vya mawasiliano.
-
-
Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali NgumuAmkeni!—2007 | Machi
-
-
Watu wengi wanakubali kwamba simu za mkononi na Intaneti zina manufaa mengi. Hata hivyo, watu wengi huona kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Profesa Donald Roberts wa Chuo Kikuu anasema kwamba wanafunzi fulani “hawawezi kumaliza dakika chache za mapumziko bila kutumia simu zao za mkononi.” Anasema hivi: “Ni kana kwamba hawawezi kutulia hadi wazungumze kwenye simu, ni kama wanasema ‘mbona kuna kimya kingi sana.’”
Vijana wengine wanakiri kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Stephanie anakiri hivi: “Mimi ni mraibu wa kutuma ujumbe wa haraka kupitia kompyuta na simu yangu ya mkononi, kwa sababu hiyo ndiyo njia kuu ya kuwasiliana na marafiki wangu. Ninaporudi nyumbani, mimi huenda moja kwa moja kwenye kompyuta na kutumia Intaneti mpaka saa tisa usiku.” Stephanie hulipa kati ya dola 100 hadi 500 kila mwezi kwa ajili ya gharama za simu. “Kufikia sasa, wazazi wangu wananidai zaidi ya dola 2,000 kwa sababu ya gharama za ziada za simu. Lakini nimezoea sana simu yangu ya mkononi hivi kwamba siwezi kufanya mambo yangu ya kawaida bila kuitumia.”
-