Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ustadi wa Kushawishi
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Gazeti World Watch lasema: “Matangazo bora zaidi ya biashara hutayarishwa kwa ustadi sana—yakiunganisha picha zenye kuvutia, nguvu, lugha tamu na kugusia hofu zetu kubwa zaidi na mambo tuyapendayo zaidi. Matangazo ya biashara yanayofanywa wakati wengi wanatazama televisheni katika nchi zilizoendelea kiviwanda hurundika mambo mengi zaidi katika dakika moja kuliko chochote ambacho kilipata kubuniwa awali.”

  • Ustadi wa Kushawishi
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Matangazo ya televisheni huonyesha picha zenye kuvutia sana. Hayo hujaribu kuburudisha, kuwa yenye kuvutia, yenye kuchekesha, yenye fumbo, au ya kihisia-moyo. Hayo hutumia watu mashuhuri na katuni zipendwazo. Mengi hutumia mambo yenye kugusa moyo ili kunasa akili zetu, labda yakikazia paka, watoto wa mbwa, au watoto.

  • Ustadi wa Kushawishi
    Amkeni!—1998 | Agosti 22
    • Wazimaji, Wapitishaji, na Wenye Kutangatanga

      Kidhibiti-televisheni (remote control) ni silaha nzuri dhidi ya matangazo ya biashara. Wengi huzima tangazo la biashara kwa kubonyeza kidude cha kuondoa sauti. Wengine hurekodi programu katika kanda za video na wanapozitazama tena, wao hupitia kijuu-juu matangazo ya biashara kwa kubonyeza kidude cha kuyapitisha haraka-haraka. Na wengine nao, hutangatanga kutoka idhaa moja hadi nyingine wakiepuka matangazo ya biashara. Wataalamu wa kutangatanga wanajua sana muda ambao matangazo yatachukua, na watarudia programu wanayotaka baada ya matangazo hayo kupita.

      Watangazaji nao hujaribu kufanya matangazo yao yasiweze kuzimwa—yale ambayo hunasa akili ya mtazamaji mara hiyo na kuishika. Hatari ya kufanya matangazo yenye kuvutia sana ni kwamba watu watakumbuka tangazo lakini watasahau bidhaa inayotangazwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki