-
Kuzikumbuka Siku za Mwisho za Yesu DunianiMnara wa Mlinzi—1998 | Machi 15
-
-
Yesu afika kwenye hekalu mapema. Jana, aliwaka hasira kwa sababu ya kule kutumia kwa kadiri kubwa ibada ya Babake, Yehova Mungu, kwa faida za kibiashara. Kwa hiyo, kwa bidii kubwa, aanza kuwatupa nje wale wenye kununua na kuuza hekaluni. Kisha apindua meza za wabadili-fedha wenye pupa na mabenchi ya hao waliokuwa wakiuza njiwa. “Imeandikwa,” Yesu asema kwa mkazo, “‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini nyinyi mnaifanya pango la wapokonyaji.”—Mathayo 21:12, 13.
Makuhani wakuu, waandishi, na watu walio wakubwa wachukizwa sana na matendo na ufundishaji wa Yesu wa hadharani. Jinsi watamanivyo sana kumwua! Lakini wazuiwa na umati kwa sababu watu washangazwa na kufundisha kwa Yesu na wafuliza “kushikamana sana naye ili wamsikie.” (Luka 19:47, 48)
-
-
Kuzikumbuka Siku za Mwisho za Yesu DunianiMnara wa Mlinzi—1998 | Machi 15
-
-
“Pango la Wapokonyaji”
YESU alikuwa na sababu ya kutosha kusema kwamba wafanya-biashara wenye pupa walikuwa wameligeuza hekalu la Mungu kuwa “pango la wapokonyaji.” (Mathayo 21:12, 13) Ili kulipa kodi ya hekalu, Wayahudi na wageuzwa-imani kutoka nchi nyingine walipaswa kubadilisha fedha zao za kigeni ili kupata fedha zilizokubalika. Katika kitabu chake The Life and Times of Jesus the Messiah, Alfred Edersheim aeleza kwamba wabadili-fedha walikuwa wakianzisha biashara kwenye majimbo katika Adari 15, mwezi mmoja kabla ya Sikukuu ya Kupitwa. Kuanzia Adari 25, waliingia katika eneo la hekalu huko Yerusalemu ili kujinufaisha na ule mmiminiko mkubwa wa Wayahudi na wageuzwa-imani. Wachuuzi waliendesha biashara yenye kusitawi, wakitoza ada fulani kwa kila kipande cha fedha walichobadilisha. Rejezo la Yesu kwao kuwa wapokonyaji ladokeza kwamba ada zao zilikuwa zenye kupita kiasi sana hivi kwamba walikuwa, kwa kweli, wakiwanyang’anya maskini fedha.
Baadhi yao hawangeweza kuleta wanyama wao wenyewe wa dhabihu. Yeyote aliyefanya hivyo ilimbidi mnyama wake achunguzwe na mkaguzi kwenye hekalu—kwa ada fulani. Wakiwa hawataki kujitia katika hatari ya kukataliwa kwa mnyama baada ya kumleta kutoka umbali mrefu, wengi walinunua mnyama “aliyekubaliwa” Kilawi kutoka kwa wachuuzi hao wafisadi kwenye hekalu. “Huko, wengi wa wakulima maskini walitozwa fedha kupita kiasi,” asema msomi mmoja.
Kuna uthibitisho kwamba Anasi, kuhani wa cheo cha juu wa zamani na familia yake walitarajia kunufaika kutokana na wafanya-biashara katika hekalu. Maandishi ya kirabi yasema juu ya “ile Minada ya [hekaluni] ya wana wa Anasi.” Ushuru kutoka kwa wabadili-fedha na kutokana na kuuza wanyama katika ardhi ya hekalu ulikuwa mojawapo ya vyanzo vyao vikuu vya mapato. Msomi mmoja asema kwamba tendo la Yesu la kuwafukuza wafanya-biashara “halikukusudiwa kuathiri tu hadhi ya makuhani bali pia chanzo chao cha mapato.” Hata sababu iwe nini, hapana shaka maadui wake walitaka kumwua!—Luka 19:45-48.
-