-
Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 1Amkeni!—2010 | Novemba
-
-
Kisha mchoro ukapatikana katika ukuta wa hekalu la Karnak (Thebesi ya kale) huko Misri.
Mchoro huo unamwonyesha Shishaki akiwa amesimama mbele ya mungu Amoni, mkono wa Shishaki ukiwa umeinuliwa akiwachinja mateka. Pia majina ya miji ya Israeli iliyoshindwa imeandikwa katika mchoro huo, na mengi ya miji hiyo inahusianishwa na maeneo yanayotajwa katika Biblia. Zaidi ya hilo, maandishi hayo yanataja “Shamba la Abramu”—na hayo ndiyo maandishi ya kale zaidi ya Misri kumtaja mzee wa ukoo Abrahamu anayetajwa katika Biblia.—Mwanzo 25:7-10.
-