Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Inaonekana kwamba Yehova alikuja kwenye hekalu lake la kiroho kwa ajili ya kuhukumu karibu miaka mitatu na nusu baadaye, katika 1918, akiandamana na Yesu akiwa “mjumbe wa agano” wake. (Malaki 3:1; Mathayo 13:47-50) Ulikuwa wakati wa kukataa hatimaye wale Wakristo bandia na kuweka rasmi ‘yule mtumwa mwaminifu na mwenye akili juu ya mali yake yote.’—Mathayo 7:22, 23; 24:45-47.

  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku katika ukurasa wa 32]

      Wakati wa Kutahini na Kuhukumu

      Yesu alibatizwa na akapakwa mafuta awe Mfalme-Mchaguliwa kwenye Mto Yordani wapata Oktoba 29 W.K. Miaka mitatu na nusu baadaye, katika 33 W.K. yeye alikuja katika hekalu la Yerusalemu akatupa nje wale ambao walikuwa wakilifanya kuwa pango la wanyang’anyi. Kunaonekana kuwa na ulinganifu wa hilo katika kile kipindi cha miaka mitatu na nusu kutoka Yesu atawazwe kuwa Mfalme katika mbingu katika Oktoba 1914 mpaka kuja kwake kukagua wale waliodai kuwa Wakristo hukumu ilipoanza na nyumba ya Mungu. (Mathayo 21:12, 13; 1 Petro 4:17) Mapema katika 1918 ule utendaji wa Ufalme wa watu wa Yehova ulikutana na upinzani mkubwa. Ulikuwa wakati wa kutahini duniani pote, na wale waoga walipepetwa wakatupwa nje. Katika Mei 1918 viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walichochea kufungwa gerezani kwa maofisa wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, lakini miezi tisa baadaye hao waliachiliwa. Baadaye, yale mashtaka ya bandia yaliyokuwa dhidi yao yaliondolewa. Tangu 1919 tengenezo la watu wa Mungu, likiwa limejaribiwa na kusafishwa, lilisonga mbele kwa bidii likatangaze Ufalme wa Yehova kwa njia ya Kristo Yesu kuwa ndilo tumaini pekee kwa aina ya binadamu.—Malaki 3:1-3.

      Yesu alipoanza ukaguzi wake katika 1918, hapana shaka viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walipokea hukumu mbaya. Hawakuwa wameanzisha tu mnyanyaso mbaya dhidi ya watu wa Mungu bali pia walijiletea hatia ya damu kwa kuunga mkono yale mataifa yaliyokuwa yakipigana katika kipindi cha ile vita ya ulimwengu ya kwanza. (Ufunuo 18:21, 24) Kisha hao viongozi wa kidini wakaweka tumaini lao katika ule Ushirika wa Mataifa uliofanyizwa na mwanadamu. Pamoja na milki yote nzima ya dini bandia ya ulimwengu, Jumuiya ya Wakristo ilikuwa imeanguka kabisa kutoka kibali cha Mungu kufikia 1919.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki