-
Kukabiliana na Tisho la UgaidiAmkeni!—2001 | Mei 22
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 10]
Ugaidi na Vyombo vya Habari
“Magaidi wanaowadhulumu watu wasio na hatia hupenda sana kutangazwa kote ili kutimiza malengo yao ya kisiasa au kubabaisha watu tu,” asema Terry Anderson, mwandishi wa habari ambaye alitekwa na magaidi nchini Lebanon kwa miaka saba hivi. “Magaidi huhisi wamefaulu hasa inapotangazwa kwamba mtu ametekwa nyara kwa sababu za kisiasa, au ameuawa au watu wamelipuliwa kwa bomu. Habari hizo zisiposambazwa ulimwenguni pote, magaidi wanahisi kwamba matendo yao ya kikatili hayakuwa na maana yoyote.”
-
-
Ugaidi Utakoma Karibuni!Amkeni!—2001 | Mei 22
-
-
Matendo ya kigaidi huwa yamepangwa kimbele na kudhamiriwa. Lengo kuu si kuua na kujeruhi watu wengi. Mauaji hayo huwasaidia kutimiza lengo lao. Magaidi huzusha hali ya wasiwasi na hofu ili kudunisha wenye mamlaka. Wao hutaka kusikilizwa na kutimiziwa mahitaji yao hususa.
-