Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Historia ya Waroma Inatufunza Somo Fulani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
    • Tertullian, mwandikaji wa karne ya tatu alisema kwamba raha ambayo watazamaji walipata, “haikupatana na dini ya kweli na utii kwa Mungu wa kweli.” Aliona watu waliohudhuria maonyesho hayo kuwa sawa na wale waliowaua wenzao.

  • Historia ya Waroma Inatufunza Somo Fulani
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Juni 15
    • [Sanduku katika ukurasa wa 28]

      Vita vya “Kutuliza Wafu”

      Tertullian, mwandikaji wa karne ya tatu anasema hivi kuhusu chanzo cha maonyesho hayo ya wapiganaji: “Watu wa kale walifikiri kwamba wanawatumikia wafu kwa kufanya maonyesho hayo yasionekane kuwa ya kikatili sana. Watu wa kale waliamini kwamba nafsi za wafu hutulizwa kwa damu ya binadamu, hivyo waliwatoa kuwa dhabihu mateka au watumwa wa hali ya chini waliowanunua. Baadaye waliona kwamba inafaa kufunika uovu huo kwa kuufanya kuwa mchezo wa kuwafurahisha watu. Kwa hiyo baada ya watu hao walionunuliwa kuzoezwa kutumia silaha za wakati huo kulingana na uwezo wao—walijifunza kuuawa!—kisha siku ya mazishi wakapigana hadi kufa kwenye makaburi. Kwa hiyo watu wa siku hizo walipata faraja ya kifo kwa kuua. Hii ndiyo asili ya munus. Baadaye, maonyesho hayo yalifikia kiwango ambacho ustaarabu na ukatili ulikuwa sawa; kwa sababu watu hawakufurahia sikukuu iwapo wanyama wakali hawakurarua watu vipande-vipande. Watu waliotolewa dhabihu ili kutuliza wafu walionwa kuwa tambiko la mazishi.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki