-
Acinipo Jiji la Kale LililosahauliwaAmkeni!—2004 | Machi 8
-
-
Ukumbi wa Pekee
Tulivutiwa tena na ukuta mrefu kilimani. Tulijiuliza lilikuwa gofu la nini katika enzi ya Waroma. Tulipolikaribia, tuligundua kwamba tulikuwa nyuma ya ukumbi mkubwa. Ulijengwa kwa mawe na ulikuwa na tao kubwa na mnara. Kulingana na desturi ya Waroma, mawe yalichongwa na kupangwa bila kutiwa saruji. Tulipoingia kupitia tao hilo, tulijipata jukwaani tukitazama viti na ngazi zilizotumiwa na watu wapatao elfu moja. Ukumbi huo ulichongwa kwenye mwamba kilimani. Tulifurahi kujua kwamba tulikuwa mahali ambapo waigizaji na wasemaji Waroma walisimama zamani!
Waroma walijua kutumia milima vizuri kwa kuichonga na kuifanya kumbi kubwa. Magofu ya kumbi za Waroma yanapatikana sehemu mbalimbali kama vile Mérida huko magharibi mwa Hispania, Trier huko Ujerumani, na Nîmes na Arles huko Ufaransa, na hata maeneo ya kaskazini kama Caerleon, huko Wales. Yale yanayojulikana sana yako Pompeii na Rome. Watu 50,000 waliketi katika Ukumbi wa Roma! Magofu ya zaidi ya kumbi 75 za Roma yametawanyika kotekote katika Milki ya Roma ya kale. Vikundi vya waigizaji vilisafiri kutoka ukumbi mmoja hadi mwingine vikiwatumbuiza watu.
Ukumbi wa Acinipo ndiyo sehemu ya jiji iliyohifadhiwa vizuri zaidi. Sehemu yake ya kuketi iko katika mwinuko kilimani na hivyo inazuiwa na pepo zinazovuma kutoka milimani. Ukumbi huo umetengenezwa kwa njia ya kwamba sauti inaweza kusambaa kwa urahisi.
-
-
Acinipo Jiji la Kale LililosahauliwaAmkeni!—2004 | Machi 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Sehemu ya nyuma ya ukumbi
[Picha katika ukurasa wa 15]
Ukumbi na jukwaa
[Picha katika ukurasa wa 15]
Mnara wa ukumbi
-