Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukristo wa Mapema na Serikali
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Mei 1
    • Kuhusu hali ngumu ya Wakristo wa mapema katika jamii ya Kiroma, mwanasosholojia aliye pia mwanatheolojia Ernst Troeltsch aliandika hivi: “Vyeo na miradi zilizohusika kwa vyovyote na ibada ya sanamu, au ibada ya Maliki, au zile zilizohusika kwa vyovyote na umwagikaji wa damu au adhabu ya kifo, au zile ambazo zingehusisha Wakristo na ukosefu wa adili wa kipagani, zote zilikataliwa.”

  • Ukristo wa Mapema na Serikali
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Mei 1
    • Profesa Troeltsch aliandika hivi: “Tangu karne ya tatu na kuendelea mbele hali ikawa ngumu zaidi, kwa kuwa Wakristo walikuja kuwa wengi zaidi katika vyeo vya juu vya Jamii na katika taaluma za juu, katika jeshi na katika ngazi za juu. Katika mafungu kadhaa katika maandishi [yasiyo ya Kibiblia] ya Kikristo mna mateto makali dhidi ya kushiriki katika mambo hayo; kwa upande mwingine, twapata pia majaribio ya kuridhiana—hoja zilizokusudiwa zinyamazishe dhamiri zisizotulia . . . Tangu wakati wa Konstantino magumu hayo yakapotea; mzozo kati ya Wakristo na wapagani ukapoa, na vyeo vyote vya Serikali vilikuwa wazi kwa Wakristo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki