-
Kupambana Sana kwa Ajili ya Habari Njema Huko ThesalonikeMnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
-
-
Jiji la Thesalonike, ambalo leo linaitwa Thessaloníki au Salonika, ni jiji lenye bandari linalositawi sana. Jiji hilo liko kaskazini-mashariki mwa Ugiriki.
-
-
Kupambana Sana kwa Ajili ya Habari Njema Huko ThesalonikeMnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
-
-
Karibu mwaka wa 315 K.W.K., Kasanda alijenga jiji katika upande wa magharibi ya Rasi ya Chalcidice na kulipa jiji hilo jina la mke wake.
-
-
Kupambana Sana kwa Ajili ya Habari Njema Huko ThesalonikeMnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
-
-
Pia, jiji la Thesalonike lilikuwa na mafanikio mengi. Jiji hilo lilikuwa na mojawapo ya bandari nzuri za kiasili katika Bahari ya Aegea. Vilevile, katika nyakati za Waroma, barabara maarufu inayoitwa Via Egnatia ilipitia katika jiji hilo. Kwa sababu Thesalonike lilikuwa katika eneo lenye bahari na barabara kuu, jiji hilo lilikuwa mojawapo ya maeneo muhimu ya kufanyia biashara na mataifa mengine katika Milki ya Roma. Kwa muda mrefu, jiji hilo lenye mafanikio lilikuwa likitamaniwa sana na Wagothi, Waslavi, Wafranki, wenyeji wa Venice, na Waturuki. Wengine wao waliteka eneo hilo kwa nguvu na kukawa na umwagaji damu.
-