-
Uzima wa Milele Duniani—Tumaini Lililofunuliwa TenaMnara wa Mlinzi—2009 | Agosti 15
-
-
Mwanatheolojia Mkatoliki Augustine wa Hippo (354-430 W.K.) “aliamini kwamba hakutakuwa na utawala wa miaka elfu,” kinasema kitabu kimoja (The Catholic Encyclopedia).a
-
-
Uzima wa Milele Duniani—Tumaini Lililofunuliwa TenaMnara wa Mlinzi—2009 | Agosti 15
-
-
6 Kabla ya kuwa “Mkristo” akiwa na umri wa miaka 33, Augustine alikuwa mfuasi wa falsafa mpya za Plato ambazo zilianzishwa na Plotinus katika karne ya tatu. Baada ya Augustine kuwa Mkristo, aliendelea kufuata falsafa hizo mpya za Plato. Kitabu kimoja (The New Encyclopædia Britannica) kinasema hivi kumhusu Augustine: “Alitimiza fungu kubwa sana katika kuchanganya kabisa mafundisho ya Agano Jipya na mafundisho ya Plato ya falsafa za Kigiriki.” Kitabu kingine (The Catholic Encyclopedia) kinasema kuwa Augustine alieleza kwamba Utawala wa Miaka Elfu unaotajwa katika kitabu cha Ufunuo sura ya 20 ulikuwa wa “mfano” tu. Kinaongezea hivi: “Maelezo hayo . . . yalikubaliwa na wanatheolojia wa nchi za Magharibi walioishi baadaye, na fundisho la mwanzoni la utawala wa miaka elfu halikuungwa mkono tena.”
-