Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na katika kiti cha ufalme zinatoka meme na sauti na ngurumo.” (Ufunuo 4:5a, NW) Lo! jinsi inavyokumbusha madhihirisho mengine yenye kutia hofu ya uwezo wa kimbingu wa Yehova! Mathalani, wakati Yehova ‘aliposhuka’ juu ya Mlima Sinai, Musa aliripoti hivi: “Katika siku ya tatu wakati ilipokuwa asubuhi, ikawa kwamba ngurumo na meme zikaanza kutukia, na wingu zito juu ya mlima na sauti kubwa sana ya pembe. . . . Wakati sauti ya pembe iliendelea kuwa kubwa zaidi na zaidi, Musa akaanza kunena, na Mungu wa kweli akaanza kujibu yeye kwa sauti.”—Kutoka 19:16-19, NW.

  • Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha Kimbingu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 15. Ni ngurumo gani ambazo zimetoka katika kiti cha ufalme katika sehemu hii ya siku ya Bwana?

      15 Kwa kawaida ngurumo hufuatana na umeme. Daudi alirejezea ngurumo halisi kuwa “sauti ya Yehova.” (Zaburi 29:3, 4, NW) Wakati Yehova alipopigania Daudi dhidi ya adui zake, ngurumo ilisemekana kuwa ilitoka kwa Yeye. (2 Samweli 22:14; Zaburi 18:13) Elihu alimwambia Ayubu kwamba sauti ya Yehova ilivuma kama ngurumo, Yeye anapofanya “vitu vikubwa ambavyo sisi hatuwezi kujua.” (Ayubu 37:4, 5, NW) Wakati wa sehemu hii ya siku ya Bwana, Yehova ‘amenguruma,’ akionya juu ya matendo makubwa ambayo atafanya dhidi ya adui zake. Hii milio ya ufananisho ya ngurumo imetoa mwangwi na ikatoa mwangwi tena na tena katika dunia yote. Wewe ni mwenye furaha ikiwa umesikiliza matangazo haya yenye ngurumo na unatumia ulimi wako katika kuongezea ukubwa wayo!—Isaya 50:4, 5; 61:1, 2.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki