Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Vitu Ambavyo Lazima Vitukie Karibuni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 11. (a) Ni kwa sababu gani ni jambo la muhimu sisi tuyashike maneno ya unabii huo? (b) Ni wakati gani ambao lazima uwe karibu sana sasa kihatari?

      11 Ni jambo la muhimu sisi tuyashike maneno ya unabii huo, “kwa kuwa wakati uliowekwa u karibu.” Wakati uliwekewa nini? Utimizo wa unabii wa Ufunuo, kutia hukumu za Mungu. Wakati uko karibu kwa Mungu na Yesu Kristo kutekeleza hukumu ya kukata maneno juu ya mfumo wa ulimwengu wa Shetani. Wakati Yesu alipokuwa hapa duniani, yeye alitaarifu kwamba baba yake pekee ndiye alijua “siku hiyo au saa.” Akitazama mbele kwenye taabu ambazo zimeongezeka duniani katika nyakati zetu, Yesu alisema pia hivi: “Kizazi hiki hakitapitilia mbali kwa vyovyote mpaka mambo haya yote yatukie.” Kwa hiyo wakati uliowekwa wa kutekeleza uamuzi wa Mungu ni lazima uwe karibu sana kihatari. (Marko 13:8, 30-32, NW) Kama Habakuki 2:3 hutaarifu: “Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia.” Wokovu wetu kuipita ile dhiki kubwa unategemea kushika kwetu Neno la kiunabii la Mungu.—Mathayo 24:20-22.

  • Vitu Ambavyo Lazima Vitukie Karibuni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Yohana anaandika hivi: “Mwenye furaha ni yeye ambaye husoma kwa sauti kubwa na wale ambao husikia maneno ya unabii huu, na ambao hushika vitu vilivyoandikwa katika huo; kwa kuwa wakati uliowekwa u karibu.”—Ufunuo 1:3, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki