Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Makaburi Hutufunulia Imani za Kale
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • Kuoza Pamoja na Wengine Kwenye Makaburi ya Kifahari

      Mnamo 1974, maskini karibu na jiji la Xi’an, huko China, walikuwa wakichimba kisima. Lakini badala ya kupata maji, walipata nyuta za shaba, vichwa vya mishale, na vipande vya watu waliotengenezwa kwa udongo. Bila kujua, walikuwa wamefukua askari-jeshi wakubwa waliotengenezwa kwa udongo miaka 2,100 iliyopita. Askari hao zaidi ya 7,000 pamoja na farasi, walizikwa wakiwa wamesimama na wamejipanga kwenye gwaride! Askari-jeshi hao wa udongo wa Ch’in ambao ni sehemu ya kaburi kubwa zaidi la kifalme huko China, wamepewa jina la Ch’in Shih Huang Ti, maliki aliyeunganisha majimbo ya China yaliyokuwa yakipigana mnamo mwaka wa 221 K.W.K.

      Kaburi la Ch’in linaweza kutajwa kuwa jumba la mfalme lililo chini ya ardhi. Lakini kwa nini alizikwa na askari hao wa udongo? Katika kitabu chake The Qin Terracotta Army, Zhang Wenli anasema kwamba “kaburi [la Ch’in] liliwakilisha milki ya Qin [nalo] lilikusudiwa kumpa Qin Shi Huangdi [Ch’in Shih Huang Ti] fahari na mamlaka aliyokuwa nayo akiwa hai wakati ambapo angekufa.” Sasa kaburi hilo ni sehemu ya jumba la makumbusho lililo kwenye eneo kubwa sana lenye makaburi 400 na mashimo yaliyo karibu nalo.

      Ili kujenga kaburi hilo, “zaidi ya watu 700,000 kutoka sehemu zote za milki hiyo waliandikishwa,” asema Zhang. Kazi iliendelea baada ya Ch’in kufa mwaka wa 210 K.W.K. na iliendelea kwa muda wa miaka 38. Hata hivyo, si msafara wote wa Ch’in uliozikwa pamoja naye ulikuwa wa udongo. Wanahistoria wanasema kwamba mrithi wa Ch’in aliagiza masuria wa Ch’in ambao hawakuwa na watoto wazikwe pamoja naye, na hivyo kusababisha vifo vya watu “wengi sana.” Kulikuwa na mazoea kama hayo katika nchi nyingine pia.

  • Makaburi Hutufunulia Imani za Kale
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 21]

      Jeshi la udongo la Ch’in, kila askari alitengenezwa akiwa na uso wa kipekee

      [Hisani]

      Inset: Erich Lessing/Art Resource, NY; © Joe Carini / Index Stock Imagery

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki