-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na yeye atateswa kwa moto na salfa katika mwono wa malaika watakatifu na katika mwono wa Mwana-Kondoo. Na moshi wa kuteswa kwao hupaa milele na milele, na mchana na usiku wao hawana pumziko, wale ambao huabudu hayawani-mwitu na mfano wake, na yeyote ambaye hupokea alama ya jina lake.”—Ufunuo 14:10b, 11, NW.
-
-
“Babuloni Mkubwa Ameanguka!”Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Wao ‘huteswaje kwa moto na salfa’? Kwa njia ya kwamba mbiu ya ukweli huwafichua na kuwaonya juu ya hukumu ya Mungu inayokuja. Kwa hiyo wao wanasuta watu wa Mungu na, inapowezekana wanashawishi kwa uayari hayawani-mwitu wa kisiasa anyanyase na hata kuua Mashahidi wa Yehova. Ukiwa upeo, wanadini hao wenye kupinga wataharibiwa kama kwa moto na salfa. Ndipo “moshi wa kuteswa kwao hupaa milele na milele” katika njia ya kwamba hukumu ya Mungu kwao itatumika kuwa kiwango cha kupimia endapo wakati mwingine wowote uhalali wa enzi kuu ya Yehova unatiliwa shaka. Suala hilo litakuwa limemalizwa kwa umilele wote.
18 Ni nani leo wanaopeleka ujumbe wenye kutesa? Kumbuka, wale nzige wa ufananisho wana mamlaka ya kutesa watu ambao hawana muhuri wa Mungu juu ya vipaji vya nyuso zao. (Ufunuo 9:5) Kwa wazi, hawa wakiwa chini ya mwelekezo wa kimalaika ndio ‘watesaji.’ Hao nzige wa ufananisho huendelea hivyo, hivi kwamba “mchana na usiku wao hawana pumziko, wale ambao huabudu hayawani-mwitu na mfano wake, na yeyote ambaye hupokea alama ya jina lake.” Na mwishowe, baada ya uharibifu wao, ithibati yenye kukumbusha kutetewa huko kwa enzi kuu ya Yehova, “moshi wa kuteswa kwao,” utapaa milele na milele.
-