-
Je, Hilo Pigano Linafanikiwa?Amkeni!—1996 | Januari 8
-
-
Zisizoonekana sana ni taka za viwanda zenye sumu, ambazo mara nyingi huzikwa mahali fulani. Ingawa hazionekani, hakuna uhakikisho kwamba sikuzote zitasahauliwa. Bado zaweza kupenyeza kwenye ugavi wa maji ulioko chini ya ardhi na kutokeza hatari za kiafya mbaya zaidi kwa mwanadamu na wanyama. “Hatujui la kufanya na kemikali zote zinazotokezwa na viwanda vya kisasa,” akakubali mwanasayansi wa Hungaria kwenye Taasisi ya Hidrolojia ya Budapest. “Hata hatuwezi kuzifuatilia.”
-
-
Je, Hilo Pigano Linafanikiwa?Amkeni!—1996 | Januari 8
-
-
Taka zenye sumu. Nusu ya kemikali 70,000 zinazotengenezwa kwa sasa zaainishwa kuwa zenye sumu. Marekani peke yake hutokeza tani milioni 240 za taka zenye sumu kila mwaka. Ukosefu wa habari hufanya isiwezekane kuhesabu jumla ya ulimwenguni pote. Kwa kuongezea, kufikia mwaka 2000, kutakuwa na tani zipatazo 200,000 za taka zenye unururishi zilizohifadhiwa katika maeneo ya muda.
-