Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Vitu vya Kuchezea vya Zamani na vya Sasa
    Amkeni!—2005 | Agosti 8
    • Kuchagua Vitu vya Kuchezea

      Gazeti The Daily Telegraph la London linasema: “Sasa vitu vya kuchezea huonyesha wazi kuwa jamii yetu ni yenye jeuri na isiyotii sheria.” Ingawa maneno hayo hayahusu vitu vyote vya kuchezea, makala moja katika gazeti la Mexico La Jornada inaonyesha kwamba ni jambo la kawaida kuona vitu vichache vya kuchezea ambavyo vimetumiwa kwa muda mrefu, na vitu vingi “vyenye maumbo ya kutisha . . . yanayoonekana kuwa ya kikatili.” Makala hiyo inamnukuu Patricia Ehrlich, ambaye ni mwalimu na mtafiti kwenye Chuo Kikuu cha Xochimilco Autonomous cha Mexico, akisema kwamba vitu vingi vya kuchezea vinavyouzwa hukazia maoni ya watu wengi ya kumiliki kwa kutumia jeuri, ukatili, mamlaka, ujitiisho, na woga.

      Shirika la Kitaifa la Wanasaikolojia wa Shule huko Marekani linaunga mkono wazo la kwamba kutumia sana vitu vya kuchezea vinavyokazia sana jeuri “kunaweza kuathiri vibaya uwezo wa mtoto wa kujifunza na kukua na kusababisha madhara.” Uchunguzi unaonyesha kwamba michezo yenye jeuri ya video na kompyuta inaweza kumfanya mtoto awe mkatili na mhalifu. Kwa hiyo, kila mtu ambaye humtunza mtoto anapaswa kufikiria kwa makini anapochagua vitu vya kuchezea vinavyofaa.—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 26.

      Kwa sababu ya maendeleo ya teknolojia ya kisasa, kuna vitu vya kuchezea vya namna nyingi na vya hali ya juu. Lakini huenda wazazi wasiwe na pesa za kuvinunua, huenda watoto wakachoshwa navyo haraka, au huenda tu visiwafae watoto. Leanne, mama mwenye watoto watano asiye na mwenzi huko Australia anasema: “Wavulana wangu wakubwa huathiriwa na matangazo ya kibiashara na mara nyingi wao huniomba niwanunulie michezo ya kompyuta iliyo ghali. Hata hivyo, wao huonekana kuwa wenye furaha zaidi wanapocheza nyuma ya nyumba kwa kutumia gongo la bei rahisi na mpira. Nimeona kwamba vitu vya kawaida vya kuchezea ndivyo hudumu zaidi na huwafanya watoto wangu watumie uwezo wao wa kufikiri katika njia nyingi.”

  • Vitu vya Kuchezea vya Zamani na vya Sasa
    Amkeni!—2005 | Agosti 8
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 26]

      Kitu kizuri cha kuchezea . . .

      ● Ni salama na kinafaa umri na uwezo wa mtoto

      ● Kimetengenezwa vizuri na kinadumu (watoto hupenda kubomoa vitu)

      ● Kinavutia na kumpendeza mtoto vya kutosha kunasa fikira zake

      ● Kinachochea uwezo wa mtoto wa kubuni na kufikiri

      ● Si ghali

      ● Hakina sumu

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki