Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Unawezaje Kujifunza Kweli Kumhusu Mungu?
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
    • Mapokeo ya Kusimuliwa—Je, Yanategemeka?

      Dini za kiasili za Waafrika hazina vitabu vitakatifu vya zamani. Mapokeo, desturi, na imani kumhusu Mungu husimuliwa kutoka kizazi hadi kingine. Kitabu West African Traditional Religion kinasema: “Huenda habari zinazosimuliwa zisiwe sahihi. Mara nyingi, mambo fulani huongezwa au kuondolewa katika habari hizo, nazo hubadilishwa au kupotoshwa, hutiwa chumvi au zinakuwa zenye kutatanisha hivi kwamba mara nyingi ni vigumu kutofautisha kweli na habari za kubuniwa.”

      Sanduku: Kitabu kimoja kinasema nini kuhusu kutegemeka kwa mapokeo?

  • Ni Nani Wanaoishi Katika Makao ya Roho?
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
    • Ni Nani Wanaoishi Katika Makao ya Roho?

      1. Dini ya kiasili imelinganishwaje na mlima?

      IMANI za kiasili za Waafrika zimelinganishwa na mlima. Juu kabisa kuna Mungu, ambaye ana nguvu nyingi zaidi za kiroho. Chini kidogo kuna miungu au roho wengine wadogo, ambao ni watumishi wa Mungu. Chini yao kuna wazazi wa kale waliokufa, ambao huzikumbuka familia zao duniani na kuzisaidia. Chini kabisa kuna roho wenye nguvu kidogo: wachawi, waaguzi, na walozi.

      2. Msemo mmoja wa Kiafrika unaonyeshaje kwamba imani za kiasili huathiri dini?

      2 Imani hizo za kiasili zimeathiri sana dini nyingine barani Afrika. Msemo mmoja wa Kiafrika unasema: “Kufuata Dini (ya Kikristo au Kiislamu) hakutuzuii kuabudu miungu yetu.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki