Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Uwe Ukijizoeza Mwenyewe”
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • Kitabu The Olympic Games in Ancient Greece kinasema: “Wale waliowazoeza vijana walitumia njia mbili hasa. Njia ya kwanza ilikusudiwa kumtia moyo yule anayejizoeza ajitahidi iwezekanavyo kushinda, nayo ya pili ilikusudiwa kuboresha mbinu na njia yake ya kushinda.”

  • “Uwe Ukijizoeza Mwenyewe”
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • Mojawapo ya majukumu ya mzoezaji wa kale ilikuwa ‘kuamua kila mwanariadha angehitaji mazoezi ya aina gani na angejizoeza mara ngapi kwa ajili la mchezo fulani,’ anasema msomi mmoja.

  • “Uwe Ukijizoeza Mwenyewe”
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • Wazoezaji wa kale ‘wangeweza kutofautisha uchovu au udhaifu uliotokana na mazoezi na ule uliotokana na hali ya akili, moyo mzito, kushuka moyo na kadhalika. Wazoezaji walikuwa na mamlaka kubwa juu ya wanariadha hivi kwamba wangeweza kuchunguza maisha yao ya faraghani na hata kuingilia kati ilipohitajika.’

  • “Uwe Ukijizoeza Mwenyewe”
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • Bila shaka, mengi zaidi ya kuwa na mzoezaji mzuri yalihitajiwa ili mwanariadha ashinde. Mengi yalitegemea mwanariadha mwenyewe na jinsi alivyojitoa kufanya mazoezi kwa bidii. Mazoezi hayo yalikuwa makali, kwa kuwa mwanariadha alihitajika kujinyima kabisa vitu kama vile ngono na pombe, na kula chakula maalum. Horace, mshairi mmoja wa karne ya kwanza K.W.K., alisema kwamba wale walioshindana “waliepuka wanawake na divai” ili “kupata ushindi waliotamani sana.” Naye msomi mmoja wa Biblia F. C. Cook anasema kwamba iliwabidi washiriki wa mashindano hayo ‘wajidhibiti na kula chakula maalum kwa miezi kumi.’

  • “Uwe Ukijizoeza Mwenyewe”
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 1
    • ‘Mpake Mafuta’

      Mpaka-mafuta alitimiza sehemu fulani wakati wa mazoezi ya wanariadha katika Ugiriki ya kale. Kazi yake ilikuwa kuipaka mafuta miili ya wanaume waliokuwa karibu kuanza mazoezi. Wazoezaji “waliona kwamba kuna manufaa fulani zinazotokana na kukanda misuli vizuri kabla ya kuanza mazoezi, na kwamba kumkanda mwanariadha kwa makini na kwa wororo baada ya kufanya mazoezi ya muda mrefu, kunamsaidia kupata nguvu tena,” kinasema kichapo The Olympic Games in Ancient Greece.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki