Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Epafrodito—Mjumbe wa Wafilipi
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 15
    • Hatujui habari nyingi, lakini twaweza kuwazia kwamba Epafrodito aliwasili Roma akiwa amechoka kutokana na safari yake. Yaelekea alisafiri kupitia Via Egnatia, barabara ya Kiroma iliyopitia Makedonia. Aweza kuwa alivuka bahari ya Adriatic mpaka kwenye “kisigino” cha rasi ya Italia kisha kupitia barabara ya Njia ya Apio hadi Roma. Ilikuwa safari ya kuchosha (kilometa 1,200 kwenda peke yake) ambayo yaelekea ilichukua zaidi ya mwezi mmoja.—Ona kisanduku kwenye ukurasa 29.

  • Epafrodito—Mjumbe wa Wafilipi
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 15
    • Taabu za Safari

      Siku hizi safari kati ya miji maarufu ya Ulaya, sawa na safari aliyofunga Epafrodito, huenda isichukue jitihada kubwa. Hiyo safari ingeweza kumalizwa kistarehe kwa ndege kwa muda wa saa moja au mbili. Ilikuwa hali tofauti kabisa kufunga safari kama hiyo katika karne ya kwanza. Wakati huo, kusafiri toka mahali hadi mahali kulimaanisha taabu. Msafiri wa miguu angeweza kutembea kati ya kilometa 30 na 35 kwa siku moja, akijihatarisha kwa hali ya hewa na hatari nyingine mbalimbali, kutia ndani “wanyang’anyi.”—2 Wakorintho 11:26.

      Vipi kuhusu vituo vya kulala usiku na ugavi wa vyakula?

      Mwanahistoria Michelangelo Cagiano de Azevedo aeleza kwamba kando ya barabara za Kiroma, “kulikuwapo mansiones, nyumba za hoteli, pamoja na akiba ya chakula, nyumba ya kutunzia na kulisha farasi, na makao ya wafanyakazi wazo; kati ya mansiones mbili zenye kufuatana, kulikuwa mutationes kadhaa, au vituo vya kupumzikia ambapo mtu angeweza kubadilisha farasi au gari na kupata ugavi.” Nyumba hizo za wageni zilikuwa na sifa mbaya sana kwani mara nyingi zilikuwa na watu wa jamii ya hali ya chini. Zaidi ya kunyang’anya wasafiri, wenye hoteli hizo waliongeza mapato yao kutokana na mapato ya malaya. Mtunga mashairi ya kuchekesha Mlatini, Juvenal, alieleza kwamba wowote waliojikuta wamelazimika kulala katika makao hayo huenda walijikuta “wakilala kando ya wauaji wakatili, katika ushirika wa wafanyakazi wa mashua, wezi, na watumwa watoro, kulala kando ya wanyongaji na watengeneza majeneza. . . . Kikombe kimoja kilitumiwa na wote; hakuna aliye na kitanda chake mwenyewe, wala meza mbali na wengine.” Waandikaji wengine wa zamani walilalamikia maji machafu ya kunywa na vyumba, vilivyokuwa na msongamano wa watu, vichafu, vyenye unyevu na viroboto wengi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki