Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mabomu ya Ardhini—Kuchunguza Athari Zake
    Amkeni!—2000 | Mei 8
    • Waungana Kukomesha Mabomu ya Ardhini

      Mnamo Desemba 1997, wawakilishi kutoka nchi kadhaa walitia sahihi Mkataba wa Kupiga Marufuku Utumiaji, Urundikaji, Utengenezaji na Uuzaji wa Mabomu ya Ardhini na wa Kuharibu mabomu hayo, pia huitwa mkataba wa Ottawa. “Hayo ni mafanikio yasiyo na kifani katika sheria ya kimataifa ya upunguzaji wa silaha au sheria ya kimataifa inayotetea haki za binadamu,” asema Jean Chrétien, waziri mkuu wa Kanada.b Hata hivyo, nchi zipatazo 60—kutia ndani baadhi ya watengenezaji mashuhuri wa mabomu ya ardhini ulimwenguni—hazijatia sahihi mkataba huo.

      Je, mkataba wa Ottawa utafaulu kukomesha kabisa tatizo la mabomu ya ardhini? Labda kwa kiasi fulani. Lakini wengi wana shaka. “Hata nchi zote ulimwenguni zikifuata mkataba wa Ottawa,” asema Claude Simonnot, mkurugenzi-msaidizi wa Shirika la Handicap International, katika Ufaransa, “hiyo itakuwa hatua moja tu katika kukomesha hatari ya mabomu ya ardhini duniani.” Kwa nini? “Mamilioni ya mabomu yangali yametegwa ardhini, yakisubiri kuwalipua watu,” asema Simonnot.

  • Mabomu ya Ardhini—Kuchunguza Athari Zake
    Amkeni!—2000 | Mei 8
    • b Mkataba huo ulianza rasmi Machi 1, 1999. Kufikia Januari 6, 2000, ulikuwa umetiwa sahihi na nchi 137 na kuidhinishwa na nchi 90 kati yake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki