Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Bado Kuna Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004 | Machi 8
    • Mwisho wa Vita Baridi

      Kulingana na kitabu The Encyclopædia Britannica, katika miaka ya 1970, Vita Baridi vilipungua “kama ilivyoonyeshwa katika mkataba wa 1 na wa 2 wa SALT [Mashauriano ya Kudhibiti Silaha za Nyuklia], wakati mataifa mawili yenye nguvu zaidi yalipokubaliana kupunguza makombora ya masafa marefu na mizinga iliyotegwa ambayo inaweza kurusha makombora ya nyuklia.” Kisha, mwishoni mwa miaka ya 1980, Vita Baridi vikapungua, na hatimaye vikamalizika.

      Ripoti ya Shirika la Carnegie la Amani ya Kimataifa ilisema hivi: “Kumalizika kwa Vita Baridi kuliwapa watu tumaini la kwamba mashindano ya kumiliki silaha za nyuklia na mabishano kati ya Marekani na Urusi yalikuwa karibu kwisha.” Kutokana na jitihada za kupunguza silaha za nyuklia, mamia ya silaha za nyuklia zimeharibiwa katika miaka ya karibuni. Katika mwaka wa 1991, Muungano wa Sovieti na Marekani zilitia sahihi Mashauriano ya Kupunguza Silaha za Nyuklia, ambao kwa mara ya kwanza ulishurutisha mataifa hayo yenye silaha nyingi zaidi za nyuklia kudhibiti na pia kupunguza makombora yaliyotegwa hadi 6,000 kwa kila nchi. Mwishoni mwa mwaka wa 2001, nchi zote mbili zilisema kwamba zimetekeleza mkataba huo kwa kupunguza makombora yao ya nyuklia kama walivyokubaliana. Isitoshe, katika mwaka wa 2002, nchi hizo zilikubali Mkataba wa Moscow uliotaka zipunguze silaha ziwe kati ya 1,700 na 2,200 katika miaka kumi ijayo.

  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004 | Machi 8
    • Kupunguza Silaha kwa Ujanja

      Gazeti Bulletin of the Atomic Scientists linasema hivi: “Zaidi ya silaha 31,000 za nyuklia bado zinahifadhiwa.” Linaongezea hivi: “Asilimia 95 ya silaha hizo zinapatikana Marekani na Urusi, na zaidi ya 16,000 zimetegwa.” Huenda watu fulani wakaona hila iliyopo katika idadi ya silaha za nyuklia zilizopo. Je, mataifa yenye silaha nyingi zaidi za nyuklia hayakusema kwamba tayari yamepunguza silaha zao hadi 6,000 kwa kila nchi?

      Hapa pana ujanja fulani. Ripoti ya Shirika la Carnegie la Amani ya Kimataifa inasema hivi: “Idadi ya makombora 6,000 inategemea njia fulani ya kuhesabu iliyokubaliwa katika Mashauriano ya Kupunguza Silaha za Nyuklia. Mataifa yote mawili yatabaki na maelfu ya silaha za ziada za masafa mafupi na nyingine akibani.” (Italiki ni zetu.) Kulingana na gazeti Bulletin of the Atomic Scientists, “makombora mengi ya Marekani yaliyoteguliwa yatahifadhiwa (pamoja na makombora 5,000 hivi yaliyo akibani) badala ya kuharibiwa.”

      Kwa hiyo, mbali na maelfu ya silaha za nyuklia zilizotegwa—ambazo zinaweza kurushwa kutoka bara moja hadi lingine—kuna maelfu ya makombora ya nyuklia na ya masafa mafupi yaliyotengenezwa kushambulia maeneo ya karibu. Bila shaka, mataifa mawili yenye silaha nyingi zaidi za nyuklia bado yana silaha tele za nyuklia katika maghala yao zinazoweza kuua watu wote ulimwenguni mara kadhaa! Kuhifadhi idadi kubwa hivyo ya silaha hatari kunaleta tisho lingine, yaani kurusha makombora ya nyuklia bila kukusudia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki