-
Lile Pigano la Kuokoa Sayari YetuAmkeni!—1996 | Januari 8
-
-
a CFC zimetumiwa kwa mapana katika mikebe ya kunyunyiza erosoli, friji, vidhibiti-hewa, visafishio, na utengenezaji wa vihami vya povu. Ona Amkeni! la Desemba 22, 1994, “Angahewa Letu Linapoharibiwa.”
-
-
Lile Pigano la Kuokoa Sayari YetuAmkeni!—1996 | Januari 8
-
-
Hata hivyo, kupiga hatua mbele kwenye kutokeza kulitukia mnamo 1987, katika Mkataba wa Montreal, uliohusisha mwafaka wa kimataifa wa kuondoshea mbali klorofluorokaboni (CFC) katika kipindi fulani cha wakati kilichowekwa.a Kwa nini wahangaike hivyo? Kwa sababu CFC zasemekana kuwa zachangia upungufu wa haraka wa tabaka la ozoni lenye kukinga la dunia. Ozoni katika angahewa la juu la dunia huchangia fungu muhimu katika kuchuja miali ya jua ya kiukaurujuani, ambayo yaweza kusababisha kansa ya ngozi na uvimbe jichoni. Hili si tatizo katika Australia tu. Hivi majuzi, wanasayansi wamechungua upungufu wa asilimia 8 katika ukolevu wa ozoni wa wakati wa kipupwe juu ya baadhi ya maeneo yenye hali-hewa ya kadiri ya Kizio-Nusu cha Kaskazini. Tayari tani milioni 20 za CFC zimepaa kuelekea tabakastrato.
Yakikabiliwa na uchafuzi huu wa angahewa wenye kuleta msiba, mataifa ya ulimwengu yaliweka kando tofauti zayo yakachukua hatua ya kuazimia.
-