Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Parachichi—Tunda Linalotumiwa kwa Njia Nyingi Sana!
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • Miparachichi inapochanua hufunikwa na maelfu ya maua ya rangi ya manjano hafifu. Hata hivyo, ni ua 1 tu kati ya maua 5,000 linalopata kuwa parachichi. Jambo la pekee kuhusu maua hayo ni kwamba kila ua huwa na stameni, au sehemu inayotoa chavua, na wakati huohuo, pistili, au sehemu inayotoa mbegu. Ua haliwezi kujichavusha kwa sababu ya utaratibu wa ajabu wa mparachichi unaotendesha sehemu hizo wakati tofauti-tofauti.

      Kama tokeo, maua ya miparachichi fulani hufunguka wakati wa asubuhi ili yapokee chavua na hufungika wakati wa mchana. Maua yaleyale hufunguka tena wakati wa jioni ili kutoa chavua. Miparachichi mingine ya karibu hufuata utaratibu ulio kinyume na huo. Uchavushaji hutukia wakati mti unaotoa chavua unapokuwa karibu na mti unaopokea chavua wakati uleule. Pia, nyuki au wadudu wengine ni muhimu katika kuhamisha chavua. Hivyo, upatano wenye kutatanisha ajabu wa nuru ya jua, wadudu, upepo, na mahali hufanikisha uzalishaji wa tunda hili.

  • Parachichi—Tunda Linalotumiwa kwa Njia Nyingi Sana!
    Amkeni!—1999 | Desemba 22
    • Karibu kila sehemu ya mparachichi ina manufaa. Mbao zake hutumiwa zikiwa fueli. Kokwa yake, au mbegu, hutumiwa huko Amerika Kusini kutia alama kwenye mavazi, kwa kuwa huacha alama idumuyo. Katika sehemu fulani za Filipino, matawi yake hutumiwa kutayarishia chai. Inasemekana kwamba gamba la mparachichi laweza kutumiwa kutayarisha ngozi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki