-
Kutafuna Chingamu Ni Zoea la Kisasa na la KaleAmkeni!—2002 | Februari 22
-
-
Waazteki walitafuna tzictli, utomvu wa mti wa sapodilla.
-
-
Kutafuna Chingamu Ni Zoea la Kisasa na la KaleAmkeni!—2002 | Februari 22
-
-
Utomvu wa mti wa sapodilla unafanana na maziwa, na mti huo unaitwa pia mti wa chingamu. Mti huo unapatikana katika msitu wa mvua unaoitwa Gran Petén, kaskazini mwa nchi ya Guatemala, katika nchi ya Belize, na katika Rasi ya Yucatán huko Mexico. Katika maeneo mengine, zaidi ya miti 75 aina ya sapodilla inaweza kukua katika ekari moja tu. Katika majira ya mvua, watu wanaokusanya utomvu huo hukatakata mashina ya miti hiyo ili utomvu utiririke polepole katika chombo kilichowekwa chini ya mti. Kisha utomvu hukusanywa, huchemshwa hadi uwe na ugumu unaotakikana, hufinyangwa na kutengenezwa kuwa vipande, na kuuzwa. Ijapokuwa utomvu huo bado hutumiwa kwa kadiri fulani kutengeneza chingamu, hasa chingamu ya asilia, tangu miaka ya 1940 chingamu nyingi hutengenezwa kwa vitu visivyo vya asili huko Marekani.
-