Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Singapore—Kito cha Asia Kilichopoteza Mng’ao
    Amkeni!—1997 | Juni 8
    • Mashtaka dhidi ya wageni yaliondolewa. Lakini 64 ambao ni wananchi wa Singapore walifanyiwa kesi mahakamani mwishoni mwa 1995 na mapema 1996. Wote 64 walipatwa na hatia. Watu 47 wenye umri kati ya miaka 16 na 72, hawakulipa faini za maelfu ya dola nao wakatiwa gerezani kuanzia juma moja hadi majuma manne.

  • Singapore—Kito cha Asia Kilichopoteza Mng’ao
    Amkeni!—1997 | Juni 8
    • Hata naibu msimamizi wa polisi ambaye aliongoza kikundi cha ushambulizi dhidi ya Mashahidi wa Yehova alikiri mahakamani kwamba hiyo ndiyo iliyokuwa mara pekee kwamba yeye na maofisa wake walikuwa wameamriwa kuvunja mkutano wa kidini. Manukuu yafuatayo yanatoka kwenye nakala za uthibitisho:

      Swali: (Kwa naibu msimamizi) Kadiri unavyofahamu je, Secret Societies Branch imepata wakati wowote kuchunguza na kushtaki vikundi vyovyote vya kidini ambavyo havijasajiliwa, isipokuwa Mashahidi wa Yehova?

      Jibu: Hakuna kikundi kingine ninachojua.

      Kisha maswali yakaendelea.

      Swali: (Kwa naibu msimamizi) Je, umepata wakati wowote binafsi kufanya shambulizi kama hilo kwa kikundi kidogo cha kidini, kilichokutana katika nyumba na ambacho hakijasajiliwa chini ya Sheria ya Sosaiti?

      Jibu: Sijapata.

      Mwito wa Kuomba Kuchukuliwa kwa Hatua

      Shirika la Kimataifa la Haki za Kibinadamu na Shirika la Kimataifa la Mawakili kila moja lilipeleka mtazamaji walo lenyewe wa kipekee ili achunguze uaminifu wa kesi hizo. Mtazamaji asiyependelea, wa Shirika la Kimataifa la Haki za Kibinadamu, Andrew Raffell, mwenyewe akiwa wakili wa Hong Kong, alisema yafuatayo: “Nasema katika ripoti yangu kwamba kesi hiyo ilikuwa na mwonekano wa mahakama bandia isiyo halali.” Yeye alieleza zaidi kwamba maofisa wa serikali walioitwa kuwa mashahidi hawakuweza kueleza mahakama kwa nini fasihi ya Mashahidi wa Yehova ilionekana kuwa isiyofaa. Raffell aliorodhesha baadhi ya vichapo vya Biblia vilivyopigwa marufuku kutia ndani Furaha—Namna ya Kuipata na Kupata Faida Zote za Ujana Wako. Yeye aliongeza kwamba havingeweza kikweli kuonwa kuwa visivyofaa katika maana yoyote ile ya neno hilo.

      Mtazamaji kutoka Shirika la Kimataifa la Mawakili, Cecil Rajendra, alitaarifu yafuatayo:

      “Tangu mwanzoni, ilikuwa wazi kwangu kwamba kesi yote ilikuwa hasa . . . wonyesho wa kipuuzi ulioonyeshwa waziwazi ili kudhibitishia ulimwengu kwamba bado demokrasia inazoewa katika Singapore.

      “Matokeo yalikuwa hakika na hakukuwa na tashwishi yoyote wakati wowote ule kabla ya, wakati wa au mwishoni mwa kesi hiyo kwamba washtakiwa wote wangepatikana na hatia kama walivyoshtakiwa.

      “Ingawa kesi hiyo ilifanywa katika mahakama ya chini na mashtaka yalikuwa uvunjaji mdogo wa Sheria ya Sosaiti hali iliyozunguka mahakama ilikuwa ya hofu na tisho.

      “Hali hiyo ilikuwa hasa kwa sababu ya uhakika wa kwamba kulikuwa na polisi wenye yunifomu zaidi ya 10 (6 ndani ya mahakama na 4 nje) kukiwa na wanaume kadhaa wa Kikosi cha Upelelezi wakiwa wamevalia kiraia na kuketi kwenye roshani.”

      Akitoa maelezo juu ya uendeshaji wa kesi yenyewe, Rajendra aliendelea kusema hivi:

      “Mwenendo wa Hakimu aliyetajwa wakati wa kipindi cha utazamaji (na vilevile jinsi ambavyo kesi yenyewe ilifanywa, kama inavyothibitishwa na nakala) ulithibitisha kwamba mengi zaidi yanatakiwa. . . . Kinyume cha kanuni zote za kesi isiyopendelea, Hakimu huyo pindi kwa pindi aliingilia kwa upande wa mashtaka na kuzuia upande wa utetezi kuhoji mashahidi wa upande wa mashtaka kuhusu vizibiti k.m. Biblia ya tafsiri ya King James, iliyotolewa na upande wa mashtaka kuonyesha kwamba washtakiwa walimiliki vichapo vilivyopigwa marufuku!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki