Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dini Zitapatwa na Nini?
    Amkeni!—2001 | Aprili 22
    • Mojawapo ya Dini Zinazolengwa

      Mashahidi wa Yehova wamekuwa mojawapo ya shabaha kuu ya mashambulizi yaliyoongozwa na Kanisa Othodoksi la Urusi. Katika Juni 20, 1996, mwendesha-mashtaka wa Moscow alianza kushughulikia kesi iliyoletwa mahakamani na Chama cha Kulinda Vijana na Dini Bandia ambacho kinapinga madhehebu. Kesi hiyo iliwasilishwa tena na tena hata ingawa ilikuwa ikiahirishwa mara kwa mara kwa sababu hakukuwa na mambo ya kuthibitisha kwamba Mashahidi walikuwa wahalifu.

      Pindi hiyo, habari za uwongo zilienezwa kote kuhusu Mashahidi. Gazeti la Urusi Komsomolskaya Pravda lenye nakala 1,200,000, lilisema hivi katika toleo lake la Novemba 21, 1998: “Kwa muda wa miaka miwili tu, Kanisa Othodoksi la Urusi limechapisha zaidi ya vitabu kumi, broshua, na vijitabu vinavyoshutumu Mashahidi wa Yehova.” Kwa nini kanisa hilo limekuwa likijaribu kuwaharibia Mashahidi sifa?

      Gazeti la Komsomolskaya Pravda liliendelea kusema kwamba, “yaelekea hasa ni kwa sababu idadi ya washiriki wa tengenezo hilo imeongezeka mara kumi zaidi katika miaka saba iliyopita, nalo Kanisa Othodoksi la Urusi, kama makanisa mengineyo maarufu, linachukia ushindani.”

      Kesi dhidi ya Mashahidi iliposikilizwa tena mapema mwaka wa 1999, habari ilisambazwa ulimwenguni kote. Kichwa kikuu cha gazeti la New York Times la Februari 11 chasema: “Mahakama ya Moscow Yachunguza kwa Makini Kupigwa Marufuku kwa Mashahidi wa Yehova.” Makala hiyo ilisema hivi: “Kesi inayosikizwa sasa katika chumba kidogo cha Mahakama ya Moscow, inachunguzwa kwa makini sana na vikundi vya kutetea haki za binadamu. Hilo linaonwa kuwa jaribio la kwanza la kutumia [Sheria ya Uhuru wa Dhamiri na Ushirika wa Kidini] kuzuia ibada.”

      Lyudmila Alekseyeva, msimamizi wa Shirika la Kimataifa la Helsinki la Kutetea Haki za Binadamu, alieleza kwa nini kesi ya Mashahidi ilikuwa ikichunguzwa kwa makini. Alisema kwamba endapo wale wanaojaribu kuwagandamiza Mashahidi wa Yehova “watashinda kesi hii,” basi “wataanza kushambulia vikundi vingine” ambavyo si sehemu ya dini maarufu. Lakini kesi hiyo iliahirishwa tena mnamo Machi 12, 1999. Lakini, tarehe 29 ya mwezi uliofuata wa Aprili, Wizara ya Haki ya Urusi ilisajili shirika la “Administrative Center of Jehovah’s Witnesses in Russia.”

      Licha ya kusajiliwa na serikali, Mashahidi na dini nyinginezo zaendelea kushambuliwa nchini Urusi na katika baadhi ya zile zilizokuwa jamhuri za Sovieti. Lawrence Uzzell, mkurugenzi wa Taasisi ya Keston huko Oxford, Uingereza, alisema kwamba “inafaa kuwachunguza Mashahidi wa Yehova” kwa sababu mambo yanayowapata “huonyesha kimbele mambo yatakayopata vikundi vinginevyo.” Kwa kweli, uhuru wa kidini wa makumi ya mamilioni ya watu umo hatarini!

      Washambuliwa Isivyo Haki

      Makuhani wakuu na viongozi wengine wa kidini waliwanyanyasa wafuasi wa Yesu katika karne ya kwanza. (Yohana 19:15; Matendo 5:27-33) Kama tokeo, ilisemwa hivi kuhusu Ukristo: “Kweli kwa habari ya farakano hili yajulikana kwetu kwamba kila mahali huwa lasemwa vibaya.” (Matendo 28:22) Kwa hiyo si ajabu kwamba, Wakristo wa kweli leo wanasemwa vibaya pia, kama ilivyo na Mashahidi wa Yehova.

      Lakini, baada ya kuchunguza mashtaka yaliyotolewa dhidi ya Wakristo wa mapema, Gamalieli, Farisayo mashuhuri na mwalimu wa Sheria, alishauri hivi: “Msijiingize katika mambo ya watu hawa, bali waacheni; (kwa sababu, ikiwa mpango huu au kazi hii ni kutoka kwa wanadamu, itapinduliwa; lakini ikiwa ni kutoka kwa Mungu, hamtaweza kuwapindua;) ama sivyo, huenda mkaonwa kuwa wapiganaji dhidi ya Mungu kwa kweli.”—Matendo 5:38, 39.

      Wachambuzi pia wamewachunguza Mashahidi wa Yehova kwa uangalifu sana leo. Wamegundua nini? Sergey Blagodarov, ambaye ni muumini wa Kanisa Othodoksi, alisema hivi katika gazeti la Komsomolskaya Pravda: “Kwa zaidi ya miaka mia moja, hakuna nchi yoyote duniani imeweza kuthibitisha kuwa Mashahidi wa Yehova ni wahalifu, au kwamba hawastahili kuwapo.”

  • Dini Zitapatwa na Nini?
    Amkeni!—2001 | Aprili 22
    • [Picha katika ukurasa wa 15]

      Kusikizwa kwa kesi huko Moscow mnamo Februari 1999. Washtakiwa (kushoto), hakimu (katikati), na waendesha-mashtaka (kulia)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki