-
Kwa Nini Tuzoee Kusema Ukweli?Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 1
-
-
Kwa Nini Tuzoee Kusema Ukweli?
ALIPOKUWA na umri wa miaka 18, Manfred alikuwa akifundishwa kazi ya ofisini.a Kampuni yao ilifanya mpango ili yeye na wanafunzi wengine kadhaa wazoezwe kwa siku mbili kila juma katika chuo fulani. Siku moja, walimaliza masomo mapema kuliko ilivyokuwa kawaida. Kulingana na sheria za kampuni, wanafunzi hao walipaswa kurudi kazini na kuendelea na kazi hadi mwisho wa siku. Badala yake, wanafunzi wengine wote walienda kujifurahisha, lakini Manfred akarudi kazini. Bila kutarajiwa, mkurugenzi wa kampuni aliyewasimamia wanafunzi hao akaja. Alipomwona Manfred, alimuuliza hivi: “Mbona hukwenda darasani leo? Na wanafunzi wengine wako wapi?” Manfred alipaswa kutoa jibu gani?
Watu wengi wanajikuta katika hali kama ya Manfred. Je, angesema ukweli au uwongo ili kuwalinda wanafunzi wenzake? Kusema ukweli kungewaletea wengine taabu na kumfanya Manfred achukiwe. Je, ni sawa kusema uwongo katika hali kama hizo? Wewe ungefanya nini?
-
-
Kwa Nini Tuzoee Kusema Ukweli?Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 1
-
-
Ushikamanifu Kumwelekea Mungu wa Ukweli
Manfred alimpa mkurugenzi wa kampuni jibu gani? Manfred alisema ukweli. Alisema hivi: “Mwalimu alituruhusu tuondoke mapema, kwa hiyo nikarudi kazini. Lakini kuhusu wanafunzi wengine, siwezi kusema kwa niaba yao. Labda unaweza kuwauliza wao wenyewe.”
Manfred angeweza kutoa jibu la werevu na lenye kupotosha ili apendwe na wale wanafunzi wengine. Lakini alikuwa na sababu nzuri ya kushikamana na ukweli. Manfred ni Shahidi wa Yehova. Unyoofu wake ulimsaidia kudumisha dhamiri njema. Pia, ulimsaidia kuaminiwa na tajiri wake wa kazi. Alipewa mazoezi katika idara ya mawe ya thamani, ambamo kwa kawaida wanafunzi hawakuruhusiwa kufanya kazi. Miaka 15 hivi baadaye, Manfred alipopandishwa cheo katika kampuni hiyo, mkurugenzi yuleyule alimpigia simu ili kumpongeza na kumkumbusha kuhusu kile kisa chake cha kushikamana na ukweli.
-
-
Kwa Nini Tuzoee Kusema Ukweli?Mnara wa Mlinzi—2007 | Februari 1
-
-
Zaidi ya hilo, tunahitaji kuchunguza ikiwa mtu anayeomba habari anastahili kupata jibu kamili. Kwa mfano, tuseme kwamba Manfred aliulizwa maswali yaleyale na mkurugenzi wa kampuni nyingine. Je, Manfred angekuwa na wajibu wa kumwambia kila kitu? Hapana. Kwa kuwa mkurugenzi huyo hakuwa na haki ya kupewa habari hiyo, Manfred hangekuwa na wajibu wa kuitoa. Bila shaka, hata katika kisa hiki ingekuwa kosa kusema uwongo.
-