Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nafurahia Sehemu Yangu ya Kufundisha Biblia Duniani Kote
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Julai 1
    • Nilikotumwa Kwanza Nikiwa Mmishonari

      Kwenye Shule ya Gileadi, tuliruhusiwa kuchagua wale ambao tungetumika pamoja nao katika kazi ya umishonari kabla ya kutumwa. Nilitumwa pamoja na Ruth Hemmig (sasa anaitwa Bosshard), dada mwenye sifa bora. Mimi na Ruth tulifurahi sana tulipotumwa Istanbul, Uturuki, nchi iliyo katikati ya Asia na Ulaya! Tulijua kwamba kazi ya kuhubiri haikuruhusiwa kisheria katika nchi hiyo, lakini tulikuwa na uhakika kabisa kwamba Yehova atatutegemeza.

      Istanbul ni jiji maridadi la kimataifa. Huko tulipata masoko yaliyojaa watu, aina bora zaidi za mapishi ulimwenguni, majumba ya ukumbusho yenye vitu vyenye kuvutia, majengo na mwambao wenye kupendeza. Lakini jambo muhimu zaidi ni kwamba tulipata watu wanyoofu waliotaka kujifunza kumhusu Mungu. Kulikuwa Mashahidi wachache jijini Istanbul na wengi wao walikuwa Waarmenia, Wagiriki, na Wayahudi. Lakini kulikuwa watu wa mataifa mengine, na ilifaa kujifunza lugha mbalimbali, kutia ndani Kituruki. Tulifurahia sana kukutana na watu wa mataifa mbalimbali waliokuwa na hamu ya kuijua ile kweli. Wengi wao wanaendelea kumtumikia Yehova kwa uaminifu.

      Kwa kusikitisha, Ruth hakukubaliwa kuendelea kukaa Uturuki, hivyo akalazimika kuondoka. Anaendelea na utumishi wa wakati wote huko Uswisi. Ingawa miaka mingi imepita, ningali ninamkosa sana kwa urafiki wake wenye kupendeza na wenye kujenga.

      Nahamia Bara Lingine

      Katika mwaka wa 1963, sikukubaliwa kuendelea kukaa Uturuki.

  • Nafurahia Sehemu Yangu ya Kufundisha Biblia Duniani Kote
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Julai 1
    • [Picha katika ukurasa wa 10]

      Mimi na Ruth Hemmig tulitumwa Istanbul, Uturuki

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki