Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ofisi ya tawi ilituma mapainia wawili, Robert Nisbet na David Norman, kuhubiri eneo hilo kubwa ambalo leo ni Kenya, Uganda, na Tanzania.

      Ndugu hao waliazimia kuhubiri habari njema ya Ufalme mpaka vijijini. Walianza kampeni yao Dar es Salaam mnamo Agosti 31, 1931 wakiwa na katoni 200 za vitabu. Kisha wakaelekea Zanzibar na baadaye bandari ya Mombasa, wakiwa njiani kuelekea nyanda za juu za Kenya. Walisafiri kwa gari-moshi, wakihubiri katika miji iliyokuwa njiani mpaka walipofika ufuo wa mashariki wa Ziwa Victoria. Kisha mapainia hao wawili wenye ujasiri wakaabiri meli na kusafiri hadi Kampala, mji mkuu wa Uganda. Baada ya kugawa vitabu na magazeti mengi, na pia kupata maandikisho ya gazeti la The Golden Age, ndugu hao wawili waliendelea na safari yao kwa gari mpaka ndani zaidi nchini.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Gray na Olga Smith waliamua kukaa Tanganyika (ambako leo ni Tanzania), naye Robert na George Nisbet wakaelekea Nairobi, Kenya. Baadaye, serikali ya kikoloni ilipomwamuru Ndugu na Dada Smith waondoke Tanganyika, walifunga safari hadi Kampala, Uganda. Hata hivyo wakati huo hali haikuwa nzuri, nao polisi mjini Kampala walikuwa wakifuatia nyendo zao. Licha ya hayo, kwa muda wa miezi miwili tu, Ndugu na Dada Smith waligawa vitabu na vijitabu 2,122 na kufanya mikutano ya watu wote mara sita. Hata hivyo, baadaye gavana akatoa amri ya kuwafukuza nchini nao wakalazimika kuondoka Uganda.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KAZI YA KUHUBIRI YAANZA TENA

      Aprili 1950, Ndugu na Dada Kilminster kutoka Uingereza, walihamia Kampala. Walihubiri habari njema kwa bidii. Walifurahi sana familia mbili, moja ya Kigiriki na nyingine ya Kiitaliano, zilipokubali ujumbe wa Ufalme.

      Kisha, Desemba 1952, Ndugu Knorr na Ndugu Henschel kutoka katika makao makuu ya Mashahidi wa Yehova mjini New York, wakazuru Nairobi, Kenya. Kwa kuwa Ndugu Kilminster hakutaka kukosa fursa ya kukutana nao, alisafiri kutoka Kampala hadi Nairobi. Ndugu Knorr na Ndugu Henschel waliwatia moyo ndugu hao na kupanga kutaniko lianzishwe Kampala. Muda usio mrefu baadaye, kutaniko hilo jipya lilianza kuzaa matunda, na kufikia mwaka wa utumishi wa 1954 kulikuwa na wahubiri kumi.

      Mwaka huohuo, Eric Cooke, kutoka ofisi ya tawi ya Rhodesia ya Kusini (ambako leo ni Zimbabwe), alizuru Afrika Mashariki na kushirikiana kwa muda na kutaniko hilo jipya mjini Kampala. Ijapokuwa akina ndugu walikuwa na mkutano wa funzo la Mnara wa Mlinzi kila juma, hawakuwa wa kawaida sana katika huduma ya Kikristo. Hivyo, Ndugu Cooke alimtia moyo Ndugu Kilminster wawe na mikutano yote ya kutaniko, kutia ndani Mkutano wa Utumishi kila juma. Ili kuitimiza kikamili zaidi kazi ya kuhubiri, Ndugu Cooke alikazia huduma ya nyumba kwa nyumba na kuwazoeza wahubiri kadhaa jinsi ya kufanya hivyo.

      Kufikia wakati huo, waliokuwa wakihubiriwa hasa ni Wazungu waliokuwa wakiishi Uganda. Hata hivyo, Ndugu Cooke alitambua kwamba watu wengi waliokuwa wakiishi Kampala walikuwa wakizungumza Kiganda. Alipendekeza kwamba ili kuchochea mioyo ya watu hao, ndugu wanahitaji kutafsiri angalau kitabu kimoja katika lugha ya Kiganda. Mwaka wa 1958 wahubiri wakaanza kutumia kijitabu “Habari Njema Hizi za Ufalme” kilichokuwa kimetafsiriwa karibuni. Hilo lilikuwa jambo lenye kutia moyo kama nini! Kazi ilisonga mbele na katika mwaka wa 1961, kulikuwa na kilele kipya cha wahubiri 19.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki